Eleza matumizi tofauti ya alama ya mkato au kipumuo

      

Eleza matumizi tofauti ya alama ya mkato au kipumuo.

  

Answers


kelvin
a) pumziko fupi katika senyensi
? Tulipofika sokoni, tulinunua mboga.
b) kuorodhesha
? Alinunua mboga, samaki, nyanya na viazi.
c) kuonyesha mwanzo au mwisho wa usemi halisi
? “Njoo kesho,”mama akamwambia.
d) kuandika anwani
? Shule ya upili Gatwe, S.L.P 160, Kerugoya.
e) baada ya kutaja jina la mtu anayepewa habari
? Daktari, ningependa kukuona.
f) kutenganisha sentensi zenye masharti
? Usipofanya kazi, usile.
g) kuandika tarehe
? Alizaliwa mwezi wa Julai, tarehe 18, 1999.
h) kuandika tarakimu zinazozidi elfu
? 1,000, 13,000, n.k.

kevowmuchiri answered the question on August 10, 2018 at 09:16


Next: Eleza njia tatu ambazo alama za dukuduku hutumika
Previous: Ritifaa au kibainishi hutumika vipi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions