Taja matumizi ya koloni/nukta mbili

      

Taja matumizi ya koloni/nukta mbili.

  

Answers


kelvin
a) kuorodhesha
? Ukitaka kuandaa samosa, unahitaji vitu hivi: unga, nyama, chumvi, mafuta na kitunguu
b) kutangulia usemi halisi
? Alimwangalia kisha akamtupia: “mshenzi.”
c) kuandika mazungumo, mahojiano au tamthilia
? MAMA :( Akiinuka.) Umechelewa wapi?
d) kutenganisha dakika na sekunde
? 9.25:05
e) kutangulia maelezo fulani
? Alipofungua mlango alishtuka: mizoga ya punda ilikuwa imetapakaa nje.

kevowmuchiri answered the question on August 10, 2018 at 09:53


Next: Eleza matumizi tofauti ya herufi kubwa
Previous: Eleza matumizi tofauti ya alama ya mshangao au hisi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions