Eleza kwa kina ufaafu wa mada "SAMAKI WA NCHI ZA JOTO" katika tamthilia ya damu nyeusi

      

Eleza kwa kina ufaafu wa mada "SAMAKI WA NCHI ZA JOTO" katika tamthilia ya damu nyeusi

  

Answers


KELVIN
? Anwani ni ya kiistiari
? Kumaanisha unyonyaji au kitu unachokitumia kujifaidi.
? Kuna samaki halisi wa nchi za joto ambao Peter anafanya bishara ya kuwauza nje ya nchi.
? Serikali ya kikoloni kuleta samaki wa aina ya sangara walioangamiza samaki asilia katika maziwa.
? Christine ni samaki kwa kutumiwa na Peter kutosheleza uchu wake. Pia daktari anamtoa mimba ili apate pesa.
? Zac pia ni Samaki kwani Anamfahamu Peter kupitia Zac
? Wavuvi ni samaki kwa vile Peter anawanunulia samaki kwa bei ya chini(kuwapunja) kAsha anawauza na kupata faida kubwa.
? Watu weusi ni samaki kwa vile wanapenda pesa na pesa ni chambo chao.
? Jagtit na Sunja kuibia nchi ya Uganda mapato ya ubadilishaji sarafu.
? Sunja kumlaghai Jagtit kwa kumpa noti ya dola 100 bandia.
? Zac na wengine wanaofanya kazi katika kampuni ya Peter ni Samaki kwani wanatumiwa naye katika biashara yake na faida kubwa ni yake.
? Deogracious pia ni samaki kwani anafanya kazi ya utumishi wa nyumbani kwa Peter.
? Nchi ni samaki kwani Peter anaiibia raslimali ya samaki na wahindi kama vile Sunjal na Jagtit wanaiibia pesa kwa kufanya biashara ya dola ya kimagendo.
? Makahaba wanaotafutwa na wazungu huko ‘half London’ pia ni aina ya samaki kwani chambo chao ni pesa.

kalvinspartan answered the question on August 15, 2018 at 12:30


Next: What is basal metabolic rate?
Previous: Eleza maudhui manne yanayojitokeza katika hadithi fupi ya samaki wa nchi za joto

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions