Eleza maudhui manne yanayojitokeza katika hadithi fupi ya samaki wa nchi za joto

      

Eleza maudhui manne yanayojitokeza katika hadithi fupi ya samaki wa nchi za joto.

  

Answers


KELVIN
Mapenzi nje ya ndoa/vyuoni/shuleni na athari zake
? Christine ni mwanafunzi wa shahada ya Sosholojia katika chuo cha Makerere. Aliye na tamaaa ya mpenzi wa kiume.
? Tamaa yake inasadifiana na kutokea mzungu Peter anayemfahamu kupitia Zac.
? Mwandishi anataka kuonyesha jinsi wasichana vyuoni wanavyojihusisha na mapenzi na watu walio na umri unaozidi wao ili wapate pesa (ushuga dadi).
? Anaonyesha ukosefu wa uwajibikaji kwa vile Christine anapopata mimba anaamua kuitungua.
? Anataka kuonyesha jinsi vijana wasivyochukulia maisha yao kwa umakini na tahadhari na hivyo kuishia kuyaharibu.
? Jinsi watu wanavyojiingiza katika mapenzi ya kupitisha muda kama vile Peter na Christine hawakuwa na lengo la kuoana.
Uzinifu
? Peter na Christine ni wazinifu kwa kufanya mapenzi ilhali hawajaoana.
? Tunafahamishwa huko ‘half London’ kuna wazungu wengine wanatafuta makahaba (ukahaba).
Uwajibikaji
? Peter hana uwajibikaji katika mapenzi kwani hamkingi Christine asipate mimba.
? Hata hivyo Peter anawajibika katika kazi yake kwani halewi akiwa kazini.
? Christine hawajibiki kwani hakubali mimba kama tokeo la vitendo vyake vya utovu wa uadilifu na kuilea bali anaamua kuiavya.
? Zac anawajibika kwa vile anamfahamisha Christine kuwa Peter ana wasichana wengine.
? Deogracius hawajibiki kwa vile hamfahamishi Christine kuhusu Peter ili amwambae.
? Miriam na Margaret hawawajibiki kwani Christine alipowaeleza nia ya kutoa mimba hakuna aliyemzuia au kumshauri dhidi ya kufanya hivyo.

Ukoloni
Mkongwe
? Serikali ya kikoloni kuleta samaki wa aina ya sangara walioangamiza samaki asilia.
Ukoloni mamboleo
? Peter kupunja wavuvi kwa kuwanunulia samaki kwa bei ya chini(unyonyaji).
? Peter kuibia nchi raslimali asili ya samaki.
? Peter kuamrisha wafanyakazi wake kama mnyapara na akipaaza sauti ya juu.
? Huko ‘Sailing Club’ kuna mahali pa wazungu na pa Waafrika.
? Jagtit na Patel kufanya biashara ya magendo ya kuuza dola na hivyo kuibia nchi mapato ambayo ingepatika kutokana na ubadilishaji halali wa dola.
? Huko Sailing Club ni mahali pa wazungu kwani ada ya juu ya kiingilio iliwafanya watu weusi kutopamudu.
Ukosefu wa ajira
? Christine kusema mtu angepata kazi ya kiserikali kwa kubahatika.
Madhila ya wafanyakazi
? Kuamrishwa-Peter Kuamrisha wafanyikazi wake kama mnyapara.
? Kufanyia kazi katika mazingira duni-ofisi kuukuu za kikoloni.
? Wavuvi wanaofanya kazi za mikono wana dhila la kupunjwa na wanaowanunulia wanaowanunulia samaki wao kwa mfano Peter.
Athari ya kumtelekeza mungu/dini
? Christine alikuwa mkristo aliyeokoka lakini aliasi imani yake.
? Hata dadake Dorothy alikuwa ameokoka lakini alikuwa mnafiki kwani alikuwa anajitia uongofu au anajificha chini ya kivuli cha dini.
? Kujitia uongofu huko kukamchochea Christine kuendelea na mapenzi na Peter.
? Christine kwa kuacha wokovu alitumbukia katika uzinifu na matokeo ni kutunga mimba na kuitungua.
? Kuavya mimba kunamwathiri kisaikolojia kwa kuhisi amekosea Mungu na kuishi na woga wa madhara ambayo angepata kutokana na uavyaji mimba huo.
Utabaka
? Peter ni wa tabaka la juu akiwa Uganda ilhali kwao Uingereza ni wa la chini la Cockney.
? Deogracius, Zac na wengine ni wa tabaka la chini.
? Huko Sailing Club ni mahali pa wazungu kwani ada ya juu ya kiingilio iliwafanya watu weusi kutopamudu.
? Watu wa tabaka la juu kama Peter wanaishi katika mitaa ya kifahari kama vile wa ‘Tankhill’.
Tamaa
? Peter kununua dola kimagendo ili aokoe pesa ambazo angalinunulia dola halali katika benki.
? Peter kupunja wavuvi ili ajipatie faida kubwa.
? Peter ana tamaaa ya wanawake. Ana wengine mbali na Christine.
? Peter ana tamaaa ya anasa kama vile zinaa, likizo Nairobi, ulevi, kula nyama choma na kunywa mvinyo na kutafuta makahaba.
? Christine ana tamaaa ya mpenzi wa kiume.
? Zac na wafanyakazi wengine wana tamaaa ya pesa ndio maana wanamfanyi Peter Kazi licha ya kudhalilishwa naye ka kuamrishwa kama mnyapara.
? Jagtit na Sunja wana tamaaa ya pesa na ndiyo sababu ya kuuza dola za kimagendo.
? Madaktari wana tamaa ya pesa na wanamtoa Christine mimba ili wazipate.
? Ami nana tamaa ya uongozi na ndiyo sababu ya kutaka kuangamiza maprofesa wanaopinga uongozi wake dhalimu.
? Christine anasema vijana wengine wana tamaa ya kuwa watu wakubwa anayoiita ndoto za kiwenda wazimu.
Umaskini
? Zac kulazimika kufanya kazi katika kampuni ya Peter akisoma.
? Deogracius anafanya kazi duni ya utumishi kwa Peter.
Uongozi mbaya
? Iddi Amin kufanya jaribio la kuangamiza maprofesa jambo lililosababisha wao kukimbilia uhamishoni.
Heshima
? Zac kuinuka na kumkaribisha Peter kiti alichokuwa anakalia.
Ushauri
? Zac kumshauri Christine kuwa Peter ana wasichana wengine lakini hakutilia maanani ushauri wake (mapuuza).
? Dorothy kumshauri Christine kuwa aliota wazungu wakimpa sumu lakini hakushaurika.
? Margaret na Miriam hawamshauri Christine dhidi ya kuavya mimba na hivyo wanapuuza wajibu wao mkubwa wa kumhifadhi ndugu.
Uavyaji wa mimba na athari zake/ukatili
? Athari za kisaikolojia kuhisi nafsi ikimsuta.
? Kuwa tasa.
? Kuwa muuaji.
? Kumkosea Mungu.
? Kufa.
Matumizi mabaya ya taaluma
? Daktari kumtoa Christine mimba ili apate pesa badala ya kumpa ushauri mwema.
Kasumba
? Zac kutamaani kuwa mmarekani mweusi kwa kupenda kuzungumza sana kama mmarekani mweusi-‘Hey man’.
? Kuheshimu wazungu kwa kuchukulia wazungu wote kama wa tabaka la juu ilhali kwao hawaheshimiwi kwa kuwa wa tabaka la chini.
? Watu wa rangi moja kuaminiana kwa mfano Jagtit kumwamini Mhindi mwenzake Sunja Patel ilhali anaishia kumtapeli.
Umuhimu wa kuwa makini
? Peter ni makini kwa kuzikagua dola hadi kupata kuna noti moja bandia.
? Jagtit hakuwa makini akipewa noti za dola na Patel ndipo akatapeliwa.
Bidii
? Zac anafanya kazi katika kampuni ya Peter akiwa angali anasoma.
? Peter ana bidii katika kazi yake na hatumii muda wa kazi kujistarehesha.
Anasa/starehe
? Ulevi k.m. uvutaji sigara, kunywa pombe, uzinzi, Peter kwenda likizo Nairobi kustarehe baada ya biashara kunoga, Christine kujipumbaza kwa mvinyo, Margaret kulewa n.k.
Utovu wa Uaminifu
? Peter ana wasichana wengine mbali na Christine.
? Christine na dadake Dorothy si waaminifu kwa Mungu.
Ulevi na athari zake
? Kusababisha Christine kuwa mzinifu.
? Uzinifu kusababisha mimba isiyotakikana.
? Unusu kaputi kutofanya kazi Christine akitolewa mimba.
Upyaro
? Peter kumita Jagtit mwanaharamu anapotaka kuchukua vipande vya noti bandia.
Unafiki
? Deogracius hamwambii kuwa Peter Peter ana wapenzi wengi.
? Dorothy kuwa na wokovu bandia na anatumia dini kama kivuli (ulokole).
? Peter kuwaonyesha Zac na Christine urafiki kumbe ataka kumtumia Christine.
? Miriam ni rafiki mnafiki kwani hamshauri Christine dhidi ya kuavya mimba.
Uhalifu
? Jagtit kumuuzia Peter dola kimagendo ilhali lilipaswa kufanywa na benki kuu.
? Sunja kumpatia Jagtit pesa bandia.
? Utoaji wanawake mamba.
Taasubi ya kiume/udunishaji wa wanawake
? Peter kutumia wanawake kama vyombo vya kujiburudisha.
? Wazungu kuwatumia makahaba kujistarehesha.
Utamaushi/ujidunishaji
? Christine anajiingiza katika mapenzi kwa ili kujipumbaza au kujidanganya kuwa mtu mwingine au kuwa dubwAsha tu- ujidunishaji.
? Anasema akiwa na na shahada angekuwa kama ng’ombe wa kizungu kwa vile hakuna ajira na ikipatikana mazingira ya kazi ni mabaya na mishahara ni duni.
? Vijana hujiingiza katika myenendo isiyofaa kwa kupoteza matumaini ya maisha ya kesho.
Uingiliaji wa mambo ya wengine
? Watu kumkodolea macho kwa kubusiwa na Peter shavuni.
? Wakasema ‘Hawa Malaya hawana aibu hata chembe’.
? Atakuambukiza ukimwi.
? Ona alivyokondeana.
Ubwana
? Deogracius ni mtumishi wa Peter.
? Wafanyakazi wa Peter anaowaamrisha kama mnyapara.
Ukengeushi
? Miriam na Christine kunywa pombe.
? Miriam kuvuta sigara.
? Mapenzi nje ya ndoa.
? Kutembea kwa wanaume.
? Uavyaji mamba.
? Christine kuacha imani yake na Dorothy kuwa mlokole.
Ukweli
? Zac kuonya Christine Peter ana wanawake wengi.



kalvinspartan answered the question on August 15, 2018 at 12:31


Next: Eleza kwa kina ufaafu wa mada "SAMAKI WA NCHI ZA JOTO" katika tamthilia ya damu nyeusi
Previous: onyesha matumizi ya tashhisi katika hadithi fupi ya samaki wa nchi za joto

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions