Taaluma ya Sintaksia inahusiana na taaluma nyingine nyingi. Fafanua

      

Taaluma ya Sintaksia inahusiana na taaluma nyingine nyingi. Fafanua


  

Answers


Yegon
1. Sintaksia na Fonolojia
Fonolijia ni uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha mahususi,pia ni jinsi vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili kujenga manenoyanayokubalika katika lugha. ( Massamba na wenzake)

Sintaksia kwa upande wake ni uchunguzi wa viambajengo vya sentensi ambavyo vimeundwa kwa kuunganisha sauti mbalimbali katika lugha husika
Mfano. Neno Aliyenitembelea ni sentensi na pia ni miungano ya sauti mbalimbali. Kwa hivyo linaweza kuchanganuliwa kifonolojia na kisintaksia.
• A|l|i|y|e|n|i|t|e|m|b|e|l|e|a|
• Baba- KIKI
• Abab- IKIK
2. Sintaksia na mofolojia

Mofolojia ni taaluma ya isimu inayoshughulikia vipashio vya lugha katika kuunda maneno[Rubanza (1996)]. Kipashio cha msingi katika uchambuzi wa kimofolojia ni nenoambalo ndilo hutumika kuunda daraja ya sintaksia.
Mfano.
• Mkulima anavuna
• Wakulima wanavuna
Katika mifano hii kuna thibitisho kwamba mofimu m na wa katika upande wa kiima zimeathiri utokeaji wa mofimu a na wa katika upande wa kiarifa.


3. Sintaksia na semantiki

Semantiki ni taaluma ya isimu inayochunguza maana katika lugha. Ili kuleta dhana kamilifu kuhusu uhusiano baina ya sintaksia na semantiki tutatumia mifano ya sentensi ifuatayo kutoa maelezo.

• Mtoto anacheza mpira uwanjani
• Mtoto uwanjani mpira anacheza
Kutokana mifano hii sentensi ya kwanza inaleta maana kutokana na mipangilio ya vipashio vyake ilhali sentensi ya pili haina maana kutokana na mpangilio mbaya wa vipashio vyake. Kwa kauli hii tunathibitisha kuwa sintaksia haiwezi kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha kwa kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya vipengele hivi vya lugha na kwa hivyo hutegemeana.



Welyekip answered the question on August 26, 2018 at 14:10


Next: Ni nini maana ya dhana Sintaksia?
Previous: Tunga sentensi yenye muundo ufuatao _RN+RT

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions