KIDAGAA KIMEMWOZEA – KEN WALIBORA 1 “ Nani kadai kwamba Afrika huru haiko huru...” (a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4) (b) Fafanua sifa nne za msemaji...

      

KIDAGAA KIMEMWOZEA – KEN WALIBORA

1 “ Nani kadai kwamba Afrika huru haiko huru...”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)

(b) Fafanua sifa nne za msemaji (alama 4)

(c) Toa mifano miwili ya mbinu za lugha katika dondoo hili (alama 2)

(d) Dhibitisha kwa kutoa mifano mahususi kutoka katika riwaya hii kuwa Afrika bado haijawa huru. (alama 10)

  

Answers


ESTHER
(i) msemaji _Balozi
(ii) msemewa-wanasokomoko
(iii) wapi-katika uwanja wa Nasaba Bora
(iv) Lini- sikukuu ya wazalendo nchini Tomoko

Sifa za Msemaji
(i) Mfawidhi katika sherehe za kitaifa huko sokomoko
(ii) Msiri mkubwa wa Nasaba Bora
(iii) Hatibu bora-alikuwa na maneno matamu
(iv) Mcheshi-aliwachekesha watu kwa maneno yake yaliyojaa chumvi
(v) Mnafiki- anamsifu Nasaba Bora ili anufaike kibinafsi
(vi) Mwenye tahadhari- hakutaka kusema jambo lolote ambalo lingehatarisha kazi yake
Zozote 4x1=4

(c) Mbinu za lugha
(i) Takriri – Neno huru limerudiwarudiwa
(ii) Kinaya- anadai kuwa afrika iko huru

(d) Afrika bado haijawa huru
(i) Unyakuzi wa Mashamba wa wanyonge kuendelezwa na viongozi kama walivyofanya wazungu km.
Nasaba Bora
(ii) Mauaji ya wanyonge wa wanaohatarisha utawala na maslahi ya
Mtemi Nasaba Bora
(iii) Viongozi kama Nasaba Bora kutumia asasi za serikali kama vile jela kunyamazisha waliodhaniwa kuhatarisha maslahi yao
(iv) Mahakama kutumiwa kama asasi ya kuendeleza utawala kwa kutoa hukumu zilizopendelea watawala kama mtemi Nasaba Bora
(v) Matabaka yalizidi kujidhihirisha na kupanuka zaidi ya wakati wa Ukooni-matajiri ambao walikuwa ni viongozi na vibaraka wao na maskini ambao ni watu wa kawaida
(vi) Lugha za kibepari kama kiingereza kuzidi kutumika katika shughuli rasmi kami vile utawala,mikutano rasmi katika shule n.k
(vii) Utegemezi wa misaada kutoka nchi za kibepari ili kufadhili miundo – mingi barani km. msaada wa kujenga hospitali ya Nasaba Bora
Mwafrika kuzidi kupokea elimu ya kigeni/kibepari.Nasaba Bora na Majisifu kupata
elimu kutoka kwa wamisheni kwa mfano Madhubuti anapelekwa Urusi,Fao anapelekwa Uingereza
(viii) Unyonyaji wa mwafrika kuzidi hata zaidi ya wakati wa kikoloni
(ix)Udhalimu kuendelezwa dhidi ya wanyonge

ESTHER STEVE answered the question on September 7, 2018 at 20:09


Next: “Huyu mwendawazimu anakuja nini kwenye sherehe hizi?Anafikiri sherehe hizi ni za watu wenye kichaa kama yeye”a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)b) Eleza tamathali...
Previous:  KIDAGAA KIMEMWOZEA : Ken Walibora 2. “Nilikwambia twende ukakataa……si kuona, tuone ndipo tuambe” (a) Weka dondoo katika muktadha wake (al.4) (b) Fafanua hulka za msemewa (al.6) (c) Taja tamadhali ilitumika...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions