Eeza ufaafu wa anwani Chozi la Heri

      

Eleza ufaafu wa anwani Chozi la Heri

  

Answers


Raphael
Chozi ni tone la maji au uowevu linalotoka machoni ambalo aghalabu hutokea mtu anapolia,kufurahi au moshi unapoingia machoni.
Heri
• Kuwepo kwa amani ,utulivu na usalama.
• Hali ya kupata baraka na mafanikio
• Afadhali/bora kuliko.
Kwa hivyo Chozi la Heri ni :
i. Chozi linaonekana bora /afadhali/nafuu.
ii. Chozi ambalo linaleta utulivu/amani/usalama-furaha
i. Ridhaa alipopatwa na janga la familia yake kuangamizwa na mali yake kuteketea aliyaacha machozi yamvamie yatakavyo,yautakase undani wake ambao ulikuwa unatuta na kutoa usaha kwa kuvunjikiwa .Uk.3
ii. Ridhaa anaiangalia hali ya Selume kuwa afadhali kuliko yake.Kilio chake ni afadhali kwani aila yake ingali hai.
iii. Ridhaa anayabadilisha mazingira ya Msitu wa Heri ya heri kutoka hali ya ukame kwa kuleta maji ya mabomba .Maeneo haya yanakuwa bora au nafuu kwani yanaanza kupata mvua.Uk.12
iv. Ridhaa alipotoka Msitu wa Mamba alijiona nafuu kwani wapwa zake –Lime na Mwanaheri walikuwa wamepata matibabu.Dadake Subira alitibiwa akapona.Mwamu wake Kaizari amepona donda lililosababishwa na kuwatazama mabinti zake wakitendewa unyama.Uk.36
v. Uk.36 Ridhaa anaona kisa cha Kaizari ni afadhali kuliko chake kwani hakuna aliyeangamia katika familia ya Kaizari.
vi. Matone mazito ya machozi yalitunga machoni mwa Mwangeka kutokana na maneno ya baba yake.Alihitaji kuliondoa komango ambalo lilikuwa limeifunga mishipa ya moyo wake.Machozi haya yaliulainisha moyo wake ukampa amani akali.Uk.52
vii. Bwana Kangata na mkewe ,Ndarine wlipohamia Msitu wa Mamba walipaona pahali hapo kuwa afadhali kwan hawakuwa na pengine pa kwenda.Walikokuwa wakiishi awali hakukuwa kwao.Uk.63 – 64
viii. Umulkheri anapokuwa katika shule ya Tangamano anaona mabadiliko mapya.Huku walimu wanatumia mbinu mpya kufundishia.Aidha ,Walimu wanaenda darasani kila mara.Si kama kwao ambako hawakuzoea kuwaona darasani.Uk.90.Shule ya Tangamano ni afadhali.
ix. Kairu anapomsimulia Umu kisa cha usuli wake,Umu anaona hali yake kuwa afadhali.
x. Machozi yanatakasa wahusika kama vile Mwanaheri.Mwanaheri anapowahadithia wenzake anadondokwa na machozi ambayo yalimsaidia kuutua mzigo wake wa uchungu uliompata.Uk. 97
xi. Chandachema alipoanza kuwasimulia akina Umu kisa chake ,chozi ambalo lilikuwa linamtiririka muda wote huu lilikatika ,akashusha pumzi ndefu,akatwaa tabasamu na kuutoa undani ambao alikuwa kaufumbika miaka hiyo yote.Uk.102.
xii. Uk.111 Ridhaa anajisemea kuwa siku Mwangeka atapata hurulaini wake itakuwa siku yake ya kumwaga chozi la heri.
xiii. Apondi anapojifungua mtoto wa kiume anatokwa na machozi ya furaha Uk. 116
xiv. Baada ya miaka mingi ya Dick kuuza dawa za kulevya ,alifaulu baadaye kujinasua kutoka kwa kucha za mwajiri wake.Alianza biashara yake mwenyewe ya kuuza vifaa vya umeme.Sasa akaanza kujitegemea kwa kuwa amejiajiri.Alikuwa amefungua ukurasa mpya katika maisha yake.Maisha yake sasa ni ya heri.Uk. 124
xv. Neema alipokuwa anampanga Mwaliko kama mtoto wake,anamkumbatia kwa mapenzi ya mama mzazi huku akidondokwa na chozi la furaha.Uk.167
xvi. Umulkheri alipomfikiria ndugu yake Dick machozi yalianza kumtiririka na wazazi wake walezi walimwacha kuupunguza mwemeo wa hisia zilizokuwa moyoni mwake.
xvii. Baada ya Mwaliko kujitambulisha kwa Umu na Dick ,Umu na Dick hawakungojea amalize.Walikimbia wote wakamkumbatia ndugu yao ,wakaanza kulia huku wakiliwazana .Haya yalikuwa machozi ya furaha kwao kwa kupatana tena wote wakiwa hai.

AMA

1. Ridhaa analia machozi ya huzuni wakati ambapo jamaa zake wakiwemo Becky, Terry, Tila na Lily Nyamvula wanateketeza. Baadaye analia chozi la heri wakati mwanawe Mwangeka anapofunga ndoa na Apondi.

2. Machozi ya huzuni yalimtoka Umulkheri alipoenda kituo cha polisi kuripoti kupotea kwa ndugu zake, Dick na Mwaliko. Baadaye analia chozi la furaha anapokutana kisadfa na Dick kwenye uwanja wa ndege.

3. Mwangeka anampoteza mkewe wa kwanza, Lily Nyamvula hivyo kujawa na machozi ya huzuni. Hata hivyo, anapata heri anapopendana na Apondi na hatimaye kufunga ndoa.

4. Watoto wa wakimbizi katika kambi wanakosa chakula hivyo kulia machozi ya njaa. Baadaye wanapata heri pale ambapo wanaletewa vyakula na mashirika yasiyo ya kiserikali na yale ya kidini.

5. Selume anajawa na huzuni na kilio baada ya kupata habari kuwa mume wake alikuwa amekwisha kuoa msichana wa kikwao hivyo hakujua pa kwenda wala kama angekutana tena na mwanawe, Sara. Hata hivyo, anapata heri Ridhaa anapomshauri na kuahidi kumtafutia kazi.

6. Neema anahuzunika kwa kukumbuka kisa cha Riziki Immaculata, kitoto alichookota na kuogopa kukichukua na kukitunza na hatimaye kukosa mtoto. Baadaye anapata machozi ya furaha/ heri anapokubaliwa kumchukua Mwaliko kama mwanawe wa kumlea.

7. Dick analazimishwa kushiriki katika biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya na Buda. Baadaye, Dick anaacha biashara hiyo na kujistawisha katika biashara ya vyombo vya mawasiliano. Anasema kuwa siku aliyokutana na Umu katika uwanja wa ndege ilikuwa siku ya heri kwani alipewa nasaha na Umu zilizomfunza thamani ya maisha.

8. Umulkheri analia machozi ya uchungu kila mara anapowakumbuka ndugu zake; Dick na Mwaliko. Baadaye analia machozi ya furaha wote wanapokutana kisadfa katika hoteli ya Majaliwa.

9. Umulkheri anapotoroka kwao baada ya nduguze kuibwa hajui anakoenda. Anamtafuta kijana ombaomba aliyemsaidia siku moja bila kuwa na matumaini ya mafanikio. Anapokaribia kukata tamaa anakutana na kijana huyo, Hazina. Hivyo, Umulkheri analia machozi yaliyojaa furaha na huzuni. Anafurahi kwa sababu Hazina alifaulu kujitoa katika maisha ya utegemezi. Anahuzunika kwa sababu huenda nduguze, Dick na Mwaliko wamechukua nafasi ya Hazina.

10. Lime na Mwanaheri wanadhulumiwa kwa kubakwa na vijana wakati wa ghasia baada ya uchaguzi. Baadaye wanapata nafuu baada ya kuhudumiwa na vijana wenzao ambao walitumwa kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa huduma za ushauri na uelekezaji.
11. Ridhaa anapatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu baada ya familia yake na mali yake kuteketezwa moto. Hata hivyo, anapata ushauri na uelekezaji kutoka kwa wataalamu mbalimbali hivyo kuweza kudhibiti ugonjwa huo.

12. Awali maisha ya Mwangemi na Neema yalijaa huzuni kwa kukosa mtoto. Wanapata heri wakati ambapo wanakubaliwa kumlea Mwaliko.

13. Chandachema anatelekezwa na wazazi wake kwa kuzaliwa nje ndoa. Analelewa na bibi yake. Bibi anapofariki, Chandachema anateseka kwa kukosa wa kumlea. Hata hivyo, anapata heri anapopelekwa katika makao ya watoto mayatima ya Jeshi la Wajane wa Kristu. Anajitahidi masomoni ili awe mwanasheria au afisa mkuu wa maslahi ya kijamii.

14. Hazina anaishi maisha ya kuombaomba mtaani na vijana wengine. Hatimaye anafanikiwa wakati ambapo serikali inawaokoa kutoka kinamasi cha uvutaji gundi na matumizi ya mihadarati. Anapelekwa shuleni ili kupewa mafunzo kuhusu mbinu za kukabiliana na changamoto za maisha.15. Lunga anaachishwa kazi na Shirika la Maghala ya Nafaka kwa kupinga uagizaji wa mahindi yenye sumu. Hata hivyo, anapata heri anapojistawisha na kutajirika kwa kilimo katika Msitu wa Mamba.

16. Kifo cha Mandu kinamwachia Apondi kilio na majonzi hata akachelea kuhusiana na mwanamume mwingine asije akafa. Hata hivyo, heri inamjia anapopendana na Mwangeka na hatimaye kufunga ndoa.

17. Wahafidhina wanakumbwa na matatizo wanapolazimika kutorokea Msitu wa Mamba kama wakimbizi kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hata hivyo, baadhi yao akiwemo Ridhaa wanabahatika kurudi nyumbani kutokana na jitihada za wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu: Oparesheni Rudi Edeni.

18. Ridhaa anahuzunika shuleni anapochukiwa, na wanafunzi wenzake kumuambaa wakidai kuwa yeye alikuwa Mfuata Mvua. Baadaye anapata heri baada ya mamake kuzungumza na mwalimu wake aliyewashauri wanafunzi hao. Hivyo, anapat
raphael answered the question on July 1, 2019 at 18:21


Next: Describe any five theories of management and explain how they can be used by managers to improve on their organizations
Previous: Describe major events in the evolution of HIV/AIDS from 1982 to date in Kenya

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions