"Mapenzi ya Kifaurongo",Kenna Wasike Mapenzi ya Kifaurongo" Mimi sijui hata kidogo ,huwa nayaona mapenzi kama ule mmea wa Kifaurongo.Huwa hai hali ikiwa shwari,na shari ikitokea ...

      

MAPENZI YA KIFAURONGO
"Mimi sijui hata kidogo ,huwa nayaona mapenzi kama ule mmea wa Kifaurongo.Huwa hai hali ikiwa shwari,na shari ikitokea yanafifia.....

(a) Huku ukirejelea hadihi hii,eleza maswala yanayojitokeza kama mmea wa kifaurongo katika hadithi hii

  

Answers


ESTHER
Mmea wa kifaurongo huwa hai hai hali ikiwa shwari na hujifia shari ikitokea

Tazama maswala yanayowafanya wahusika kufurahi kutaka kutaka kufanya kitu au kudhani haii ni shwari kisha hali ikibadilika wanaathirik

- Anapokuwa darasani Denis anaona hali nzuri ya wanafunzi wenzake waliosomea katika shule za mikoa na kitaifa.Tunaambiwa wana vipakatalishi na ipad lakini anahisi uchungu na kujihurumia anapokumbuka hali yake ya umaskini inayomfanya kutoshiriki vicheko na minong'ono na wenzake darasani.
- Wanafunzi wanahamu ya kuielewa somo la fasihi la Dkt.Mabonga lakini wanaishia kuachama kwa mshangao.Msichana anayeuliza swali anaiishia kubezwa na Dkt.Mabonga.Tunaambiwa anawatia hofu wanafunzi walio na hamu ya kuelewa somomla fasihi na wengi kuishia kutaka kuenda kufanya kazi zao badala ya kushiriki somo la Fasihi chuoni.
- Dennis anajaribu kuwasaidia wanafunzi wenzake kwa kumwomba Dkt Mabonga kutumia lugha rahisl lakini anazimwa anapouliza swali lake na kuchekwa hivyo basi ananyamaza.
- Dennis anapotaka kunywa uji wake alioutayarisha chumbani mwake, mlango wake unabishwa.Anashtuka na kushindwa kama aufungue au asiufungue.Anatetemeka hadi ikijasho chembamba kumteremka usoni.
- Penina anatoka katika tabaka la kitajiri.Yaonekana kuwa kwake hali ni shwari.Lakini anajifia kama kifaurongo anapokumbuka kuwa hana mpenzi pale chuoni.Tunaambiwa Analia anapokuwa chumbani kwa Dennis.
- Dennis na Penina wanaishi katika mtaa wa Newzealand.Hali yaonekana nzuri lakini tunaambiwa Dennis anaona haya kwani kodi ya nyumba yalipwa na wazazi wa Penina.
- Dennis anapoenda kwenye usaili wa kazi katika shirika la kuchapisha magazeti, anaonekana mwenye matuaini hadi mwanamke mmoja, tunaambiwa kirumbi cha mtu anapompita bila kumsalimia kisha mawazo ya kujidunisha yanamwingia akailini.
- Matumaini ya Dennis ya kupata kazi yalimjaa akilini hadi alipogundua kuwa msichana aliyekuwa naye chuoni,Shakila,ni bintiye mkurugenzi wa shirika hilo.
- Nyaraka za Dennis zaonyesha yeye ni mwanafunzi bora chuoni, lakini anapoulizwa swali na mkurugenzi anakuwa kama mmea wa kifaurongo na kushindwa kujibu swali hilo na kuishia kukosa kazi.
- Kwa kukosa kazi uhusiano wake na Penina unaathirika.Penina anamweleza alimpenda akifikiri atapata kazi lakini kwa kuwa hana kazi anatamatisha uhusiano wao.Mapenzi yao yaliyokiuka utabaka yanajifia.
- Dennis anapofukuzwa nyumbani kwa Penina anamatumaini kuwa Penina atabadilsha nia, lakini matumaini hayo yanajifia Penina anapomwambia nyumba hiyo aione paa.


ESTHER STEVE answered the question on November 12, 2018 at 09:48


Next: Why do central banks raise intrest rates?
Previous: "Penzi lenu na nani? . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!" (a) Eleza muktadha wa dondoo hii...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions