Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea

      

Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.)

  

Answers


samuel
? Imani anatafuta haki ya kunyimwa malezi ya wazazi wake waliouliwa kinyama. Imani anatafuta &aid. ya familia yake iliyonyanganywa shamba lao.

? Amani anatafuta haki ya Ami yake Yusufu.

? DJ anatafuta haki baada ya kushambuliwa na jibwa lake Nasaba Bora.

? Amani anatafuta haki ya mswada uiiokataliwa na wachapishaji na baadaye kuchapishwa kwa jina la mtu mwingine.

? Chwechwe Makweche anatafuta haki ya kuumia michezoni bila kufidiwa.

? Watoto wa Majisifu wanalilia haki ya kuishi kama binadamu wengine licha ya ulemavu wao.

Amani anatafuta haki ya kudhulumiwa na mtemi Nasaba Bora kwa kizingizio kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mkewe Bi Zuhura. Amani atafuta haki ya kujua waliokuwa wazazi wa kitoto Uhuru baada ya yeye kulazimishwa kukilea licha ya kuwa hakuwa babake.

Amani na Imani wanatafuta haki ya kufungwa kwa kizingizio kuwa walimwuua mtoto Uhuru. Wanafunzi wa mwalimu Majisifu wanatafuta haki ya kufunzwa vyema baada ya Mwalimu wao kutohudhuria shule kwa muda mrefu. Yusufu anatafuta haki baada ya kusingiziwa kumwuua Chichiri Hamadi.

? Raia wa Sokomoko wanatafuta haki dhidi ya Nasaba Bora anayewapokonya ardhi, mall, mabiruti na wake wao.

? Wafungwa wanatafuta haki kwa kukosa kufikishwa mahakamani.

? Waandishi wengi chipukizi kama Amani wanatafuta haki ya kazi zao baada ya kuibiwa miswada yao na akina Majisifu.
lemass answered the question on February 1, 2019 at 08:55


Next: Wasemao husema, atafutaye hachoki."? Haya ni maneno ya msimulizi yanamhusu:(a) Fafanua muktadha wa dondoo hill
Previous: Lakini waliogopa...waliogopa hata kuwa na uoga.”(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions