K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea“Usinivue nguo kwa macho yako wee!” Kwa kurejelea hoja kumi na mbili kutoka kwenye riwaya hii, thibitisha kwamba mzungumzaji anastahili kuvuliwa nguo.

      

K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea

“Usinivue nguo kwa macho yako wee!”

Kwa kurejelea hoja kumi na mbili kutoka kwenye riwaya hii, thibitisha kwamba mzungumzaji anastahili kuvuliwa nguo. (alama 12)

  

Answers


samuel
- Dondoo limetolewa uk. 21. Mtahiniwa aonyeshe mambo ambayo Nasaba Bora ametenda, ambayo ni ya aibu/dhuluma/ ya kumfanya ashutumiwe. Kuvua nguo- kuona uozo/kuangaza uovu/kusutwa kwa uovu Baadhi ya hoja ni:

Mauaji — Nasaba Bora kumuua Chichiri Hamadi
Uzinzi - Kuhusiana kimapenzi na Lowela.
Kuwafuta Wafanyakazi kwa makosa yasiyo na msingi kama vile kunadhi?sha mazingira Kuwapokonya Chichiri Hamadi na Mama Imani shamba.
Kuchoma nyumba ya akina Imani Kumpiga Amani kikatili Kudharau watu Wenye mahitaji maalum.
Anapogundua yule msichana ni kilema anahizika, hamtaki mapenzi tena.
Kumuua paka kikatili Kuwatoza raia
kodi kumpeleka mwanawe ng’ambo Kumwachia mkewe upweke; ati anakwenda kusuluhisha mi gogoro ya mashamba, anashindwa hata kutekeleza majukumu ya unyumba
Kumtupa mtoto wake kibandani mwa Amani
Kumpagaza Amani ulezi
Kumtafutia mwanawe kazi kwanjia ya ki?sadi,
kughushi hatimiliki
Anamwacha mwanamke azalie njiani licha ya rai za mkewe.
Anashindwa hata kusoma hotuba ya rais kwenye sherehe muhimu.
Anachangia matumizi mabaya ya pesa zilizotengewa ujenzi wa hospitali, wanaishia kujenga zahanati.
Anamlazimisha Amani kumchimbia kaburi angali hai.
Anashindwa kukabiliana na hali ya ushinde; anajiua/anakufa kifo cha aibu. Anashindwa hata kuhusiana na ndugu yake.
Anasahau mafundisho ya kidini ya baba yake. Uongozi wake unawatelekeza wazalendo kama vile Matuko Weye na Chwechwe Makweche katika ugonjwa na hali duni. U?sadi.
Anajitengenezea faili ili kupata mali akiwa mkuu katika Wizara ya Ardhi.
Anamtarajia ndugu yake Majisifu kuandika habari zake kwenye gazeti japo kwa kweli hastahiki.
Anamtaliki mkewe kwa tuhuma ambazo hajathibitisha.

lemass answered the question on February 1, 2019 at 10:06


Next: Lakini waliogopa...waliogopa hata kuwa na uoga.”(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
Previous: K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea Kwa kurejelea hoja kumi na nne kutoka kwenye riwaya hii, thibitisha kwamba raia wa Tomoko walistahili kuogopa hata kuwa na uoga‘

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions