Fafanua sehemu kuu za uandishi wa ripoti ya utafiti

      

Fafanua sehemu kuu za uandishi wa ripoti ya utafiti.

  

Answers


Edwin
1. Kichwa cha ripoti Ripoti lazima iwe na kichwa cha habari; kichwa hicho huandikwa kwa maelezo machache. Mambo muhimu yanayotakiwa kuwepo katika kichwa cha ripoti ni:

mahali pa tukio
aina ya tukio
tarehe ya tukio
muda wa tukio

2. Utangulizi wa ripoti Utangulizi wa ripoti hueleza kwa muhtasari lengo la ripoti kama ni kutoa taarifa au kumbukumbu.

3. Kiini cha ripoti Kiini cha ripoti kina maelezo yote kuhusiana na tukio lenyewe; sehemu hii huelezewa kwa ufasaha mambo yaliyotokea, chanzo chake, ukubwa wake, wahusika, na tukio linalohusika.

4. Mwisho wa ripoti Hii ni sehemu ya mwisho ya ripoti. Sehemu hii huonyesha mambo makuu mawili:

maoni ya mwandishi wa ripoti
jina la mwandishi wa ripoti na cheo chake
Nchoga answered the question on March 24, 2019 at 10:48


Next: Explain the features of social structure
Previous: Outline major reasons why there is slow growth of credit card business in Kenya

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions