Chakula cha mkulima, ni maharage na sima Mtazame mkulima, hapendezi hana dhima Bali huyu mkulima, ndiye chanzo cha uzima Maisha ya mkulima, ni ya dhiki na nakama Kibanda cha...

      

Chakula cha mkulima,
ni maharage na sima
Mtazame mkulima,
hapendezi hana dhima
Bali huyu mkulima,
ndiye chanzo cha uzima

Maisha ya mkulima,
ni ya dhiki na nakama
Kibanda cha mkulima,
huvuja na kutetema
Mgongo wa mkulima,
daima umeinama
Bali huyu mkulima,
ndiye mama wa uzima

Mke wake mkulima,
si wa pambo, wa huduma
Huyu mke mkulima,
hana muda wa kusoma
Halalami mkulima,
hunywa maji ya kisima
Bali huyu mkulima,
ndiye nguzo ya uzima

Nafasi ya mkulima,
aghalabu ni ya nyuma
Magarini mkulima,
hadhi yake kusimama
Hadharani mkulima, huambiwa hana jema
Bali huyu mkulima,
ndiye nguvu ya uzima

Elimu ya mkulima,
si kusoma si kupima
Lugha yake mkulima,
si kizungu ni ya mama
Sayansi ya mkulima,
kupanda nyanya na nduma
Bali huyu mkulima,
ndiye raha va uzima

Hunyanyaswa mkulima,
ofisi akijitoma
Anabezwa mkulima,
na watu waliosoma
Akiumwa mkulima,
hata dawa wamnyima
Bali huyu mkilima.
ndiye ngao ya uzima

Huyo ndiye mkulima,
mjueni mkulima
Akigoma mkulima,
nani atakayepuma?
Namsitu mkulima, adhaniwaye wa nyuma
kumbe huyu mkulima.
ndiye chanzo cha uzima







maswali

a) Eleza dhamira ya shairi hili

b) Taja na kueleza mikondo yoyote miwili inayojitokeza katika shairi hili

c) Taja na kueleza mbinu zozote tatu za lugha zinazojitokeza katika shairi hili

d)Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari
e) Eleza maana ya msamiati ufuatao

i)Anabezwa.

ii)Akijitoma

iii)Atakayepuma 
iv) Hadhi


  

Answers


Davis
 a).Mwandishi anakejeli umma/jamii ambayo haitambui bidii ya mkulima
b) (i). Tarbia - Mishororo minne kila ubeti
(ii) Mathnawi-. Vipande viwili / migao miwili
(iii) Mtiririko - Vina vya kati na mwisho vinatiririka
C (1). Takriri- Neno mkulima kurudiwa/ kukaririwa.
ii) Tashbihi -Mkono wa mkulima ni mgumu kama chuma
(iii) Taswira_ Picha va namna mgongo wa mkulima ulivvoinama.
(iv). Chuku - Mkono ulivyo mgumu kama chuma
v). Nidaa - Hata dawa wamnvima!
Vi) Balagha -Nani atakayepuma?
d). Maisha ya mkulima ni ya taabu na husikitisha, makao yake ni ya duni naye
amedhoofika kimwili ilhali huyu mkulima ndive mtu muhimu katika maisha.
e). (i) Anadharauliwa
(ii) Aklllingiza/ Akilitia
(iii) Atakaveishi
iv) Heshima
Githiari answered the question on April 10, 2019 at 17:54


Next: A ball is thrown horizontally from the top of a building and lands 100 m from the foot of the building. If the building is 60...
Previous: A certain animal has no incisors no canine 6 premolars and 6 molars in its upper jaw.Ln the...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions