Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki.

      

Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki.

  

Answers


Kavungya
TUMBO LISILOSHIBA.
(i) Viongozi kuweka vitego na vikwazo vya sheria ili watu wadogo wasiweze kutetea mali zao.
(ii) Kutowahusisha maskini katika maamuzi muhimu yanayoathiri maisha yao.
(iii)Kunyakua ardhi ya madongoporomoka ambapo watu maskini waliishi.
(iv) Kupanga njama za kuwapatia wanyonge visenti vichache ili waondoke madongoporomoka.
(v) Jitu la miraba mine kula chakula chote bila kubakishia wateja.
(vi) Wanamadongoporomoka kubomolewa vibanda vyao na mabuldoza.
(vii) Askari wa baraza kutimua watu waliokuwa wanabomolewa .
(viii) Jeshi la polisi kulinda askari wa baraza wakibomoa vibanda vya wanamadongoporomoka.
ix) Askari kuwapiga virungu watu.

SHIBE INATUMALIZA.
(i) Mzee mambo kulipwa kwa vyeo viwili alivyovifanyia kazi.
(ii) Waajiriwa kwenda kazini na kukosa kufanya kazi.
(iii)Viongozi kuibia wananchi kwa kujipakulia mshahara
(iv) Waajiriwa wawili kufanya kazi moja – Sasa na Mbura ni mawaziri wa wizara moja.
(v) Mzee mambo kuandaa sherehe ya kuingiza watoto nasari kwa kutumia pesa za umma.
(vi) Mzee mambo kuandaa sherehe kwa kutumia rasimali za nchi- magari, vyakula.
(vii) Sasa na mbura kula vyakula vyao na vya wenzao.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 05:21


Next: (a) Define the two theories that have been advanced to explain the origin of agriculture (b) Highlight any seven reasons..
Previous: Onyesha jinsi maudhui ya utabaka na mapenzi ,yanavyojitokeza katika hadithi ya mapenzi ya kifaurongo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions