a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
Msemaji ni Dkt Mabonga
Msemewa - Wanafunzi wa somo la fasihi
Mahali – Ukumbi wa mhadhara
Sababu – Dkt Mabonga anasuta wanafunzi kwa kuwa vitegemezi baada ya mwanafunzi kutaka kueleza namna fasihi inaelekeza
b) Taja na ufafanue tamathali ya usemi uliyotumiwa katika dondoo hili
Tashbihi- Si kama watoto wakembe
c) Hadithi hii inadhihirisha utegemezi wa binadamu. Fafanua
Dennis Machora na wanafunzi wenzake wanangojea Dkt Mabonga amjibu mwanafunzi ili nao wapate kujua
• Dkt Mabonga alisema kuwa binadamu wanapiga ubwete na kugeuka kupe
• Dkt Mabonga alisema kuwa binadamu hatafuti chakula
• Wanafunzi wengine wanaonelea waache masomo waende kusimamia biashara za wazazi wao
• Msichana mmoja alisema kwamba mchumba wake ni katibu katika wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia, kwa hivyo karibuni watafunga ndoa aondokewe na adha ya masomo
• Penina alikuwa anatumiwa Sh. 5000/-= kila wiki na wazazi kwa matumishi
• Aidha Dennis Machora alikuwa anategemea makupo wa shule kujihikimu. Pesa hizo zinapoisha anahangaika
• Dennis Machora aliona kuwa Penina angekuja kulalamika kuwa Dennis Machora amekuwa kupe.
• Penina alisema kuwa hangeweza kuolewa na mwanamume asiye na kazi yenye mshahara mkubwa.
• Dennis Machora na msimulizi waishi katika mtaa wa New Zealand na kodi ilikuwa inalipwa na wazazi wake Penina
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 05:28