TUMBO LISILOSHIBA
• Eneo la Madongoporomoka ndiko wanamoishi watu wepesi wasio na mashiko
• Watu wa Madongoporomoka walikuwa maskini
• Katika eneo la Madongoporomoka kulikuwa na mkahawa mshenzi wa Mzee Mago
• Bi Suruti alishangaa kwa kuuliza kuhusu wanachojali matajiri kuhusu maskini kama wao
• Huko Madongoporomoka kuna mashonde ya vinyesi, vibwagizo wa choo, uchafu unaonekenya, vibanda uchwara na majichafu
• Tunaambiwa kuwa watu wengi waliokuwa wamelala waliamka na kutoka nje ya vibanda vyao haraka
MAPENZI YA KIFAURONGO
• Dennis Machora alisema kuwa umaskini uhostakimu kwao haukuwa na mfano
• Dennis Machora alisema kuwa wazazi wake hawakuwa na mali ya kuwarithisha
• Dennis Machora hana chakula, inabidi apike uji usiokuwa na sukari
• Dennis Machora alikuwa na kijiredio na ametandika kitandani shuka zilizozeeka na kuchanikachanika
• Penina alimwangalia msimulizi kwa huzuni yamkini alitelewa na hali yake duni
• Dennis Machora alimwambia Penina kuwa hawawezi kuwa na usuhuba kwa kuwa Dennis anatoka kutoka familia ya umaskini naye Penina anatoka kwenye familia yenye nafasi
• Kwa kuwa Penina alimshinda Dennis Machora kiuchumi angejidunisha na Penina angemwona kama kupe
• Penina alimwita Dennis Machora kama mkata
• Penina alimwambia Dennis kuwa Mungu angempa mpenzi mwingine aupakati ufukara wake aliouzoea
• Mwanafunzi aliyekuwa na pesa angelipa kujinasibisha na mwenzake maskini
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 05:31