a) Weka dondo katika muktadha
Maneno ya wanafunzi wa shule ya Busulala.
Akimwambia Rasta/ Samueli Matandiko.
Walipokuwa shuleni.
Samueli alikuwa ametoka katika afisi ya mwalimu mkuu kuchukua matoke yake ya mtihani. Marafiki waliomjua wanamtaka awaelezee alama zake.
b) Taja mbinu zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili
i)Utohozi ii)nidaa
c) Ni kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe?
Mwalimu mkuu wa shule ya Busukalala hakuwahi kumwamini Samueli hata siku moja kama anaweza kufaulu mtihani
Mwalimu mkuu hakuamini Samueli aliposema kuwa amelipa ada mpaka alipohakikisha kwa kuangalia nyaraka na kumbukumbu zake.
Anamwonyesha Samueli dharau kwa mumrisha karatasi kama mbwa; anarejelea kile alichokuwa akifanya na kumpuuza.
Mwalimu mkuu hakumpa ushauri wowote Samueli ambo unmgemsaidia kupokea matokeo yake ambayo hayakuwa mazuri hata kidogo.
Mwalimu mkuu alimjibu Samueli kwa karaha, alipomwita kuwa ni fidhuli. Anamjibiza kwa kuuliza iwapo wanafunzi wengine wanalipa mawe au majani.
d) Je, mtihani wa maisha ni amwani faafu ya hadithi hii.
i. Mtihani wa Maisha ni anwani ambaayo imesawiri maudhui ya hadithi hii kwa kiwango kikubwa.
ii. Samueli anafanya mtihani wake wa shuyle ya upili na kuend kuyachukua matokeo. Kabla ya kufikia zamu zake Samueli anajichjunguz na kujipima uwapo ameufanya vizuri. Mawazo kuhusu mtihani huo yanamtawala.
iii. Alianza kuwachunguza wanafunzi waliokuja kuchukua matokeo ya mtihani wanaopotoka mlangoni ili kujaribu kuona iwapo wamefaulu au la.
iv. Samueli anajaribu kujiaminisha kuwa yeye atakuwa amefaulu mtihani wakati akiwa kwenye foleni ya kuchyukua matokeo.
v. Samueli anajiaminisha kuwa yeye ni mjanja na angemshangaza mwalimu mkuu.
vi. Anagundua kuwa amefli mtihani huo. Safu za alama ya D na ilimkodolea macho. Herufi hizo zilimfedhesha na akalwmewa.
vii. Nyumbani baba yake aliyengoja matokeo kwa hamu hakuyapata.
viii. Samueli anadanganya kwamba ana salio la karo.
ix. Baba anarauka na kutembea kilomita sita kwenda kuchukua matoke ya mtihani.
x. Anapogundua ni uwongo anapandwa na ghamiza.
xi. Samueli anaamua kujitosa bwawani ili aondokane na athari za kufeli mtihani huu wa kitaaluma. Hata hivyo amaokolewa na mpita njia.
xii. Mama yake anamwambia kuwa ingawa amefeli mtihani wa shule, asikate tama, bado ana mtihani wa maisha ambao anaweza kufaulu. Anwani hii ina faa sana.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 05:37