• Mhusika Mashaka aliopata mikasa mingi maishani mwake tnagu alipozaliwa. Kwanza mama yake Ma Mtumwa alifariki alipomkopoa tu, kutokana na kifafa cha uzazi.
• Babake yake naye upweke ulimshinda akafariki na wakazikwa pamoja.
• Mashaka hakuwahi kuwaona hata kwa sura, hivyo hawakumbuki.
• Biti Kidebe ndiye aliyemlea kwa shida na makuzi yalikuwa ya taabu – makuzi ya tikitimaji au tango kuponea umande.
• Biti Kidebe alikuwa haishi kulalamikia miguu yake iliyomuuma. Hivyo, licha yay eye kumlea Mashaka, naye Mashaka akamlea huyu bibi. Alitafuta kila aina ya vijikazi alivyoviweza tangu akiwa motto.
• Biti Kidebe aliwahi kumsomesha kwa shida hadi darasa la nane.
o Alipomaliza shule tu Biti Kidebe akafariki na kumwach mpweke.
• Siku moja akiwa anapiga gumzo na rafiki yake Waridi mlango ulifunguliwa ghafla wakafungishwa ndoa ya mkeka.
• Mashka anapata mke akiwa hana chochote.
• Waliowavamia chumbani mwake ni Mzee Rubeya baba yake Waridi, Sheikh Mwinyumvua, kaka yake Waridi Mansuri na rafiki yake Idi.
• Ndoa hii ilimita Rubeya aibu kwa kuwa binti yake ameolewa na fukara. Mzee Rubeya na familia yake wakaamua kurudi kwao Yemeni.
• Mashaka na Waridi waliishi katika mtaa wa watu wa hali ya chini (fukara) uitwao Tandale.
• Mandhari ya chumba chao kimoja yalikuwa kando ya choo kilichofurika vibaya wakati wa mvua na kueneza kinyesi kila mahali.
• Kulikuwa na uvundo uliotisha kwenye nyumba yao daima.
• Chumba chao kilivuja wakati wa mvua. Wakati huu wanapata tabu sana.
• Mashaka na Waridi walipata watoto saba. Hivyo ilikuwa shida watu tisa kuishi kwenye chumba kimoja.
• Mashaka alikuwa na kazi duni yenye mshahara wa mkia wa mbuzi – alikuwa mlinzi wa usiku katika kampuni za Zuia Wizi Security (ZWS)
• Watoto wake wavulana walilala jikoni kwa jirani Chakupewa.
• Watoto wake wakike walilala chini ya sakafu kwenye mkeka; Mashaka na Waridi walikuwa na vitu vichache sana maana hawakumudu kununua vyombo.
• Nafasi ilikuwa duni kabisa. Ilibidi mkewe apikie nje ya chumba chao isipokuwa, nyakati za mvua ambapo jiko huwekwa juu ya kinu kuzuia maji yanayotiririka.
• Dhiki nyumbani mwa Mashaka ndiyo ilikuwa nguo na harufu yao. Walikuwa na dhiki kubwa sana.
• Siku moja Mashaka aliporudi kutoka kazini alikuta Waridi ametoroka na watoto wote. Toka wakati huo hakuwaona tena. Akabaki mnhyonge na mpweke zaidi.
• Utengano huo ulimfanya ajutie ufukara wake na kuuona kuwa ni udhia mkubwa maishani.
• Mashaka mengi yalijikita akilini mwake kuhusu ukuta na pengo kubwa lililopo katika jamii kati ya walio nacho na wasio nacho.
• Kutokana na shida yake alikuwa na mawazo mazito na maswali yasiyo na majibu – kwa nini jumuiya za kimatiafa zinafumbia macho suala la ufukara?
• Ni ufukara uliomtenginsha yeye na Waridi, yeye na watoto wake na kumwacha katika lindi la maumivu.
• Mashaka alijipa moyo kuwa subira huenda ikamletea heri. Hata hivyo, aliendelea kusubiri akitarajia kuwa mambo yatabadilika. Lakini mambo hayakubzadilika.
• Wakati mwingine aliota ndoto kuwa pengo kati ya maskini na matajiri limepungua, na Waridi mkewe amemrudia Na wote wanaishi kwa furaha. Taabu zake zimepungua mno.
• Kumbe hayo yote ni ndoto. Akalazimika kuamka na kupanbana na ulimwengu wake wa mashaka ya umaskini.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 05:40