Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

"Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!" a) Eleza muktadha wa dondoo hii. b) Taja na ufafanue mbinu...

      

"Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!"
a) Eleza muktadha wa dondoo hii.
b) Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
c) Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyo jitokeza katika hadithi nzima.
d) Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo.

  

Answers


Kavungya
a) Eleza muktadha wa dondoo hii.
Mzungumzaji ni Penina. Anamzungumzia Dennis Machora (msimulizi)
Wako nyumbani kwao (Machora na Penina) katika mtaa wa New. Zealand.
Dennis Machora alikuwa amerudi nyumbanikutoka kampuni ya kuchapisha magazeti
alikoenda kutafuta kazi lakini akaambuliapatupu.

b) Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
Methali - Mgomba Changaraweni haupandwi
ukamea
Swali balagha - penzi lenu na nani?
Nidaa . . . Mkata wee!
Msemo - potelea mbali.
Mdokezo (.....)

c) Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyo jitokeza katika hadithi nzima.
Maudhui ya Utabaka.
• Wazazi wa Dennis walijitahidi kumsomeshakwa kuwalimia matajiri mashamba.
• Wazazi wa Penina walipinga uhusiano waDennis na Penina kwa kuwa laitoka tabaka la chini ilhali wao walikuwa matajiri.
• Dennis anakunywa uji kama chamcha kwakukosa chakula ilhali Penina hupokea shilingi elfu tano kila wiki.
• Dennis hangejiunga na shule aliyoalikwa kwa umaskni ilhali wenzake walisomea shule za hadhi kubwa.
• Penina anapangiwa nyumba katika mtaa wa New Zedand. wanakoishi watu wenye mapato ya Kadri.
• Penina anamkataa Dennis kwa kuwa hana uwezo wa kifedha kwa kukosa kazi na hangeweza kudumisha maisha yake ya kifahari.
• Wazazi wa Dennis walimtegemea asome ili kuwatoa umaskinini ilhali wazazi wa Penina wanamkimu hata baada ya kumaliza masomo.

d) Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo.
• Msaliti - Alimsaliti mchumba wake Dennis kwa kumfukuza na kuwaibisha sababu ya umaskini.
• Mwenye dharau - alimfokea Dennis kwadharau akimwita mkata.
• Mwenye tamaa - ana tamaa ya mapenzi na akatafuta mchumba kwa bidii.
• Mwenye bidii masomoni – alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha kivukoni.
• Ni jasiri - alimwendea Dennis kutafata mapenzi na uchumba na mambo yanapokwenda kombo anamfukuza bila woga.
• Mpyaro - alimtusi Dennis akimwita mkata
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:04


Next: Find the variance and standard deviation of 3, 5, 7, 9, 11
Previous: P and Q are two points such that OP = i + 2j + 3k and OQ = 4i + 5j – 3k. M is...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions