“ Mwandishi wa haditi ya Tumbo lisiloshiba ametumia mbinu ya Jazanda kwa ufanisi mkubwa.” Thibitisha

      

“ Mwandishi wa haditi ya Tumbo lisiloshiba ametumia mbinu ya Jazanda kwa ufanisi mkubwa.” Thibitisha

  

Answers


Kavungya
• Tumbo kubwa linalokula bila kujaa ni Jazanda ya vitendo vya matajiri wenye tama ajabu ya kunyakua bila kukoma mali ya maskini
• Jitu la miraba minne ni jazanda ya matajiri wakubwa ambao wanatumia nafasi yao kuwakandamiza maskini. Unene ni Jazanda ya uwezo wa kifedha na mamlaka
• Jitu linaingia kimiujiza bila kujulikana. Kuingia kwa ghafla ni Jazanda ya jinsi matajiri hawa wanavyovamia na kunyakua mali ya maskini bila kutarajiwa. Ardhi ya Wanamadongoporomoka inavamiwa bila wao kutarajia
• Jitu kukalia meza inayoweza kutoshea watu wane ni Jazanda ya matajiri kuvamia na kunyakua ardhi/mali ya maskini wengi. Ardhi inayotumika na maskini wengi inanyakuliwa ili kukidhi mahitaji ya matajiri wachache.
• Kiti kulalamika na meza kuonekana ndogo ni jazanda ya dhuluma na ukatili wa matajiri hawa kwa wananchi wenye uwezo mdogo. Maskini wanalalamika dhuluma za matajiri wanaporaji.
• Jimwili na tumbo kubwa lililolalia meza ni jazanda ya utajiri na uwezo wao wa kifedha. Tumbo kubwa pia ni jazanda ya uroho/ulafi wa mali;hawatosheki.
• Jitu kubwa kufagia chakula chote hotelini na kuwamalizia wengine ni jazanda ya jinsi amabavyo matajiri wanaparamia mali/ardhi ya wananchi maskini bila kuwabakishia chochote .
• Jitu kuja kula katika hoteli uchwara ya mzee Mago ni jazanda ya jinsi matajiri yangekuja kuinyakua ardhi ya maskini
• Kitendo cha jitu kula na kuramba sahani ni jazanda ya ulafi wa matajiri tapeli ambao tamaa yao haiwezi ikamithilishwa na chochote. Jitu linaletewa chakula kwa duru kadhaa ishara kuwa halishibi. Matajiri wenye uroho wa mali ya maskini hawakinai mpaka wanapofilisisha maskini.
• Radi inayoandamana na mstari mkali wa fedha na mweso unaopwesa na kumulika mioyo ya watu ni uelewa ambao wananchi maskini wanakua nao kuhusu kudhulumiwa kwao na walio na uwezo serikalini. Baadhi ya wanajamii kama Mzee Mago wanaelewa fika kinachoendelea. Mago analiona jinni lililokuwa hotelini kwenye gari aina ya Audi Q7 likimdhihaki ishara kuwa linatumia uwezo walo kunyakua ardhi ya maskini.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:08


Next: The sector below has a radius of 12cm and an angle AOC = 60o is folded to form a cone. Find the volume of the...
Previous: Find the equation of the normal to the tangent of the curve y=x3 – 3x2 + 2x + 1 at the point where x=3. Leave...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions