“… Ningeondoka shuleni mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.” a) Eleza muktadha wa maneno haya b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza c) “ Kinaya kimetumika...

      

“… Ningeondoka shuleni mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.”
a) Eleza muktadha wa maneno haya
b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza
c) “ Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu.” Thibitisha

  

Answers


Kavungya
a) Eleza muktadha wa maneno haya
• Haya ni maneno ya Jairo. Anahutubu katika sherehe ya kumuaga mwalimu Mosi ambaye alikuwa anastaafu kutoka kazi ya ualimu. Sherehe hii ilifanyika shuleni. Jairo anamkosoa mwalimu Mosi kwa kumpatia matumaini ya uongo masomoni ilhali alijua hawakuwa na uwezo wa kimasomo badala ya kumruhusu aende ajaribu mbinu nyingine ya kujikimu kimaisha ili awe mtu wa maana katika jamii.

b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza
Jairo anamkosoa mwalimu kwa kumfunza na kumpa matumaini maishani badala ya kumwachilia mapema aende akaibe na kuua. Jairo analodokeza hapa ni kuwa ili mtu awe wa maana ni lazima aibe au aue.

c) “ Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu.” Thibitisha
• Ni kinaya kwa Jairo kudai ili mtu awe wa maana, athaminiwe na kuitwa mheshimiwa na kuwa bingwa lazima aibe,apore au aue.
• Ni kinaya kwa Jairo kuuona uelekezi na ushauri wa mwalimu wake kama upotoshi na upotezaji wa muda. Jairo anadai alipotezewa muda kwa kupatiwa matumaini ya uongo.
• Ni kinaya pia kwa MwalimuMosi kutaka ahutubie mtu ambaye atamkosoa badala ya kumsifu.
• Ni kinaya kwa Jairo kuona elimu haina manufaa yeyote ilhali wenzake walifaidi kutoka kwa elimu ya mwalimu wao.
• Ni kinaya kuwa baadhi ya wanaofunzwa shuleni na walimu waadilifu wanaendeleza ufisadi na uporaji. Jairo anasema wenzake kama Baraka, Festo, Mshamba na Nangeto ni wakora na utajiri wao ni zao la ukora
• Ni kinaya kwa jairo kumtoa bintiye na mkewe kama zawadi kwa mwalimu wake kama shukrani ya zawadi anazompa. Ni kinaya kwa mtu kubadili mkewe kama zawadi .
• Ni kinaya kwa jairo kudai kuwa pombe ni kiliwazo cha kimawazo kinachomsahaulisha masaibu ya maisha na kumkosoa mwalimu wake kwa kumwonya dhidi ya matumizi ya pombe.
• Ni kinaya kwa mkewe Jairo kukukubali kitendo cha mumewe Jairo kumtoa kama zawadi kwa familia nyingine. Anakubali kubadilishwa na mali.
• Ni kinaya kwa jairo kudai kuwa ufuska ndio raha ya maisha na kuwa uadilifu haufai. Anadai kuwa maisha ni bora bila nasaha za mwalimu.
• Ni kinaya kwa mkewe mwalimu Mosi,Sera kukubali na kumkaribisha mwanamke mwingine na watoto wake kwenye familia yake.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:12


Next: Without using mathematical tables or calculator; evaluate:
Previous: Find the midpoint of the straight line joining A (2, 1) and D (6,5).

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions