“ Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.” Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano.

      

“ Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.” Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano.

  

Answers


Kavungya
• Mzee Mmabo anatumia uhuru wa cheo chake serikalini vibaya kwa kupokea mishahara kutoka wizara mbalimbali ilhali hafanyi kazi yoyote.
• Sasa na Mbura wanatumia uhuru wao vibaya kwa kupanga na kupangilia wapi kwa kudoea badala ya kushiriki katika shughuli ya ujenzi wa jamii.
• Wananchi wa taifa la Mzee Mambo wanatumia uhuru wao vibaya kwa kuzingatia kwenda kazini bila kujali kama wanafanya kazi yoyote. Muhimu si kwenda kazini ila kufanya kazi.
• Mzee Mmabo anatumia uhuru wake vibaya kwa kutumia mali na wakati wa taifa kuandaa sherehe zisizo na msingi wowote. Anaandaa sherehe kubwa kwa madai ya kusheherekea kuingizwa kwa mtoto wake “nasari”.
• Mambo anatumia magari ya serikali kuhudumu katika sherehe yake.
• Walaji katika sherehe ya kuingizwa kwa mtoto wa kwanza wa Mzee Mambo nasari wanatumia uhuru wao wa kula vibay kwa vile hawachunguzi kile wanachokula.
• Vyombo vya habari vinatumia uhuru wao vibaya kwa kupeperusha sherehe ya kibinafsi moja kwa moja, badala ya kumulika mambo yanayoathiri taifa.
• Sasa na Mbura wanatumia uhuru wao wa kula kila kitu kibaya na kizuri, wanachokijua na wasichokijua, vyao na vya wenzao hata vya kuokotwa. Hili linawaweka katika hatari ya kuptwa na maradhi kama kisukari na saratani.
• Dj na wengine wenye nafasi katika taifa wanatumia uhuru wao kupokea mabilioni ya pesa za serikali kutumbuiza katika sherehe za mtu binafsi.
• Dj na wenzake wanatumia uhuru wao kupata huduma za maji, umeme, matibabu miongoni mwa huduma nyingine bila malipo huku wananchi wakilazimika kulipia huduma hizi kwa dhiki na ufukara.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:13


Next: Find the midpoint of the straight line joining A (2, 1) and D (6,5).
Previous: Read the poem given below and answer the questions that follow. THAT OTHER LIFE

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions