“Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tunakula” (a) Eleza mukadha wa dondoo hili. (b) Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika. (c) Eleza umuhimu wa mnenaji. (d) “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza”...

      

“Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tunakula”
(a) Eleza mukadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika.
(c) Eleza umuhimu wa mnenaji.
(d) “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza” Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli hii.

  

Answers


Kavungya
(a) Eleza mukadha wa dondoo hili.
(i) Mnenaji ni Mbura.
(ii) Mnenewa ni Sasa.
(iii) Wakiwa nyumbani kwa Mzee Mambo.
(iv) Walikuwa wamehudhuria sherehe kwa Mzee Mambo bila ualishi katika siku ya kusherehekea siku ya kuingia darasa la chekechea kwa mtoto wa Mzee Mambo na mwingine kutoa vijino viwili. Wanafika shereheni kula, hata hivyo wanakula kilafi mpaka Mbura anaanza kujilaumu pamoja na mwenzake Sasa, kwamba wanakula vyovyote wavipatavyo bila kuvichunguza na hata kuvila vya wenzao waliowatangulia na watakaozaliwa.

(b) Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika.
Istiari / Jazanda - Wanakula lakini hawawezi kumaliza kula - wanakula kila leo na bado wanaendelea kula.

(c) Eleza umuhimu wa mnenaji.
Umuhimu wa mbura.
(i) Ni mfano mzuri wa watu walafi katika jamii.
(ii) Ni kielelezo cha watu wanaofanya kazi ngumu na nzito lakini kufaidi mapato duni.
(iii) Ni mfano wa watu walio na mapuuza. Wanafahamu uzembe uliopo miongoni mwa wafanyikazi wa serikali na unyakuzi wa mali ya umma, lakini hawachukui hatua mwafaka.
(iv) Ni kielelezo cha wanyonge katika jamii: Wanafaidi mabaki baada ya matajiri kujitwalia vyao.
(v) Ni mfano wa watu wanaojitolea kulihudumia taifa lao hata kama wametengwa mbali na hawatambuliwi katika taifa lao

(d) “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza” Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli hii.
(i) Vingozi wa mataifa yanayoendelea kutowajibikia kazi zao. Wanakubali bidhaa duni kurudidikwa katika mataifa yao: mchele wa basmati.
(ii) Mali ya umma kunyakuliwa: DJ anafungua duka la dawa zilizotolewa katika bohari ya serikali huku wanyonge wakiteseka.
(iii) Serikali kuwalipa watu ambao hawafanyi kazi mishahara kubwa hivyo kudhoofisha uchumi wa nchi - Mzee Mambo.
(iv) Kituo cha televisheni ya taifa kutumika kupeperusha matangazo ya sherehe ambazo hazina umuhimu wowote katika ujenzi wa taifa.
(v) Wananchi wengine badala ya kuchukua hatua mwafaka dhidi ya wanyakuzi, hungojea wakati wao ili nao wanyakue: Sasa na Mbura “... na sisi tuende - tusogee.
(vi) Viongozi wananyakua mali ya mabilioni kwa hila na hawajali: Mzee Mambo anaandaa sherehe kubwa kwa sababu mtoto wake wa kwanza ameingia shule ya chekechea na yule wa mwisho ameota vijino viwili.
(vii) Watu walio karibu na viongozi kupewa vyeo ilhali wanyonge hawana kazi: Mzee Mambo ana vyeo viwili.
(viii) Wanyonge kufanya kazi ngumu na nzito kwa malipo duni: Sasa na Mbura; ilhali viongozi hawafanyi kazi bali wanapakua misharaha minono: Mzee Mambo.
(ix) Viongozi kutowajibika katika kuchunguza utenda kazi wa wafanyikazi wao kwani hushinikiza wafanyi kazi kwenda kazini na sio kufanya kazi. Jambo
linalohujumu uchumi wa taifa.
(x) Wananchi kuchangia kuzorotesha uchumi wa nchi zao kwa kufumbia macho unyakuzi unapoendelezwa na viongozi: Sasa na Mbura.
(xi) Viongozi kutochunguza ubora wa vyakula vinavyoletwa shereheni. Vyakula vyenyewe vinaweza kuwa hatari kwa afya ya binadamu.
(xii) Magari ya serikali kutumika katika sherehe za kibinafsi badala ya kuwahudumia wananchi. Magari haya yanabeba mapambo; kupeleka watoto kuogeshwa katika sherehe ya Mzee Mambo.
(xiii) Watu kunyongana na kuuana ili wapate shibe hasa katika mataifa yanayoendelea.
(xvi) Wenye hadhi ya chini kuruhusiwa kuvitwaa vyao baada ya mabwanyenye kujinyakulia vyao. Wafanyavyo Sasa na Mbura.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:20


Next: The equation of a circle centre (h, k) is 2x2 + 2y2– 8x + 5y + 10 = 0. Find the values of h and...
Previous: Make y the subject of the formula given

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions