Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Hapana cha ala, bwana. Liswmwalo lipo,kama halipo linakuja. Kumbuka msemo mabrafu wa siri ya kata iulize mtungu . Mtungi wenyewe ni mimi ……” a) Eleza muktadha...

      

“Hapana cha ala, bwana. Liswmwalo lipo,kama halipo linakuja. Kumbuka msemo mabrafu wa siri ya kata iulize mtungu . Mtungi wenyewe ni mimi ……”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha tamathali mbili za lugha zilitotumiwa katika dondoo hili
c) Fafanua sifa moja ya msemaji inayodokezwa na dondoo hili
d) Msemaji wa mabo haya baadaye anageuka kata na kupiga mbizi mtungini. Eleza ukitoa mfano kutoka hadithi.
e) Eleza maudhui ya malezi kama yanavyojotokeza katika hadithi ya shogaka Dada ana Ndevu .

  

Answers


Kavungya
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
i) maneno ya Bi. Hamida
ii) akimwambia Bwana Masudi
iii) kitandani wakingojea usingizi uwachukue.
iv) wanazungumza kuhusu Mkadi, mtoto wa Habiba Chechei ambaye wanasema awe na tabia mbaya

b) Bainisha tamathali mbili za lugha zilitotumiwa katika dondoo hili
i) methali- lisemwalo lipo kama halipo linakunja.
ii) Siri ya mtungi iulize kata.
ii) tashbihi – kata iulizwe
iii)jazanda / istiari – kata, mtungi

c) Fafanua sifa moja ya msemaji inayodokezwa na dondoo hili
Mbeya/ mdaku/kilimdimi
kumsengenya mkadi kuwa ana tabia mbaya.

d) Msemaji wa mabo haya baadaye anageuka kata na kupiga mbizi mtungini. Eleza ukitoa mfano kutoka hadithi.
i) Hamida alianza kumchunguza mwanawe Sofia.
ii) Alianza kumshuku mwanawe kuwa ana mimba alimwona akitapika.
iii) Alimuuliza mwanawe ikiwa anaumwa na ikiwa ameenda hospitalini.
iv) Aliyashuku mabadiliko ya mwili wa mwanawe ijapokuwa hakuwa na ashahidi

e) Eleza maudhui ya malezi kama yanavyojotokeza katika hadithi ya shogaka Dada ana Ndevu .
i) Malezi yana changamoto kubawa kwa wazazi. Watoto wao wanawadanganya – Safia kudanganya kuwa kimwana ni shogake anayekuja wasaidiane kudurusu kumbe ni mvulana.
ii) Wazazi wa najisifu kuwa wanawapa malezi mazuri watoto wao – wazazi wa Safia kujidai wanampa malezi mazuri Safia.
iii) Wazazi wanawaamini watoto wao kiasi cha kuwa hawachunguzi mambo wanayowafanya watoto. Wazazi wa Safia.
iv) Wazazi wanaamini kuwa wanawalea watoto wao kulingana na dini- Bw. Masudi anaamini kuwa Safia ni mwenye staha. Anaogopa Mungu na wazazi wake kwa kufuata sharia na amri alizoamrisha mungu kupitia dini.
v) wazazi wanawasengenya watoto wa wengine – Bi Hamida kusengenya Mkadi mtoto wa Habiba Cheche kusema kuwa tabia zake siyo nzuri.
vi) Wazazi wa kike/ kina mama licha ya kuwaamini watoto wao wa kike bado ni wadadisi wanachofunza tabia zao za watoto wa kike.
vii) Wazazi wa Sofia wanamruhusu Safia kujifungia chumbani mwake na shogake ili wasome vizuri bila kusumbuliwa na Lulu. Hili linawapa nafasi nzuri ya kufanya mapenzi.
viii) Wazazi wanaachwa katika hali ya masikitiko baada ya watoto wao kufa.- wazazi wa Safia.
ix) Wazazi wanapaswa kujihadhari na kuwasifia watoto kwa vitendo vyao vya kinafiki. – wazazi wa Safia wanamsifia kwa kuwasaidia , kufanya kazi zozote , hodari shuleni na kujiongoza. N.k
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:25


Next: Make y the subject of the formula given
Previous: X and Y are two variables such that Y is partly constant and partly varies inversely as the square of X. If Y = 3...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions