Jadili maudhui ya elimu katika Diwani ya Tumbo lisiloshima ukizingatia hadithi zifuatazo: a) Mapenzi ya kifaurongo b) Shagake dada ana ndevu. c) Mamake Bakari . d) Mwalimu mstaafu. e) Mtihani...

      

Jadili maudhui ya elimu katika Diwani ya Tumbo lisiloshima ukizingatia hadithi zifuatazo:
a) Mapenzi ya kifaurongo
b) Shagake dada ana ndevu.
c) Mamake Bakari .
d) Mwalimu mstaafu.
e) Mtihani wa maisha.

  

Answers


Kavungya
a) Mapenzi ya kifaurongo
Maudhui ya elimu.
Elimu ya sekondari inaonyesha utabaka.Wanafunzi wa shule za kitaifa na mikoa ni wa tabaka la juu. Wazazi wao wana uwezo wa kugharamia masomo yao. Wale wa shule za vijijini ni wa tabaka la chini. Wana matatizo ya karo kwa sababu ya umaskini.
- Utabaka pia unadhihirika katika elimu ya chuo kikuu cha kimkoni, wanafunzi wenye fedha wanadharau wenzao maskini.
- Elimu ya chuo kikuu inatatiza kwa kutowajibika kwa wahadhiri katika kazi yao. DKt Mabonga anakataa kuwajibu wanafunzi wake na kuwatamausha kiasi cha kutamani kukamilisha elimu haraka wakashughulikie mambo mengine.
- Mapenzi huathiri matokeo ya mitihani ya mwanafunzi katika chuo kikuu. Dennis alifuzu vyema kwani mwanzoni hakuwa na mpenzi na hivyo alizingatia masomo.
- Elimu ndio njia ya pekee ya kumpatia mtu ajira. Dennis anatafuta kazi baada ya kukamilisha masomo.
- Elimu ndio njia ya pekee ya kumpatia mtu ajira. Dennis anatafuta kazi baada ya kukamilisha maneno.
- Elimu ina jukumu la kutengeneza mustakabali wa maisha. Dennis anataka kusoma ndio awe profesa au daktari.
- Elimu ina jukumu la kuwashauriwanafunzi kujitegemea . dkt Mabonga anawahimiza wanafunzi kujitegemea sio kuwa kupe( anasuta ukupe)
- Umaskini unachangia mwanafunzi kujiingiza katika mapenzi ya mapema .Dennis alijiingiza katika uchumba na penina kwa sababu ya umaskini.
- Umaskini unamwathiri mwanafunzi kisaikolojia kama Dennis alikuwa akiwaza kila wakati.
- Wazazi wanamatarajio makuu kwa watoto wao kuwa watawafaa baadaye ya kukamilisha elimu.

b) Shagake dada ana ndevu .
• swala la elimu limeshughulikiwa na mwandishi wa hadithi hii
• Mwandishi anadhihirisha kwamba bila kutia bidii masomoni wanafunzi hawawezi kufaulu masomoni.
• Umuhimu wa majadiliano miongoni mwa wanafunzi katika maandalizi ya mtihani.
• Safia na kimwana wanasoma pamoja.
• Hadithi inalenga umuhimu wa wazazi kufuatilia jinsi ambavyo watoto wanavyosoma.
• Wazazi wanaonywa dhidi ya mapuuza – safia analeta mwanaume nyumbani ana jifunika buibui akidai ni shogake.wakiwa katika chumba wanashiriki mapenzi na Safia kuambulia ujauzito.
• Mtoto anayesoma vizuri ni chanzo cha furaha na fahari kwa wazazi. Wazazi wa Safia wanamwonea fahali kutokana na bidii yake masomoni.
• Elimu pia inasisitiza kupita mtihani – Safia na kimwana wanadurusu pamoja kujitayarisha kupita mtihani.

c) Mamake Bakari .
katika hadithi hii elimu inaonekana kukubwa na changamoto mbalimbali.
i) Watoto wa kike kubaguliwa na walimu pamoja na wanafunzi baada ya kuwa wajawazito. Sara anaogopa kufukuzwa shuleni na mkuu wa shule.
ii) Kuwadharau na kuwadunisha wasichana wanaobeba mimba wakiwa shuleni.
iii) Badala ya walimu kuwapa ushauri nasaha wanawapiga vijembe na kuwadhihaki.
iv) Umuhimu wa bidii katika masomo sara na rafiki yake Sarina wanasoma masomo ya ziada
v) Twisheni inayofanyika usiku inahatarisha usalama wa wanafunzi .hili ndilo lililosababisha kubakwa kwa Sara.

d) Mwalimu mstaafu .
i) ni chombo cha ajira. Wanafunzi waloifunzwa na mwalimu Mosi waliishia kuwa madaktari, marubani, wahadisi na wahasibu.
ii) elimu ina jukumu la kujenga uhusiano mwema baina ya wanajamii. Mosi anaujenga uhusiano/ mkabala mwema na wanafunzi wake – hii ndiyo sababu anapostaafu wanafunzi shuleni kumzawadi.
iii) ina dhima ya kukuza vipaji vya wanafunzi. Wanafunzi waliimba na kucheza zeze, marimba, violini, vinubi, kucheza drama na sarakasi siku ya kustaajafu kwa mwalimu Mosi.
iv) kuendeleza utamaduni wa jamii mbalimbali. Wanafunzi waliimba nyimbo mbalimbali siku ambayo mwalimu Mosi alistaafu.
v)Ni chombo cha kuwaheshimu wanajamii – waliohutubu kwa kubaguana . anawalaumu kwa kutowajua watu wa matakaka yote nafasi ya kuzungumza.
vi) ni chombo cha kuwaheshimisha wanajamii – waliohutubu walimsifu Mosi kwa sababu ya kuwafunza na kuwaelekeza ipasavyo.
Vii) elimu ina jukumu la kuadilisha wanafunzi. Mwalimu Mosi aliwaandilisha wanafunzi wake kama Jeiro kwa kuwasihi kutoshiriki ufuska na kunywa pombe.
Elimu ina wajibu wa kuandaa mustakabali wa wanafunzi. Walihudhuria hafla ya kumuaga mwalimu Mosi kwa sababu alichangia pakubwa kuwafanya kuwa watu bora waliopuuza Kama Jiro hawakufua dafu

e) Mtihani wa maisha .
i) katika elimu baadhi ya walimu huwapuuza wanafunzi haswa wanapokosa kufanikiwa kimasomo. Mwalimu mkuu alimpuuza Samuel kwa sababu ya kuanguka mtihani.
ii) ulipaji wa karo ni muhimu katika elimu. Babake Samuel tayari amelipa karo, kwa hivyo hatarajii Samuel kukatazwa matokeo.
iii) elimu inashughulikia jinsi wasichana na wavulana wanasoma mf. Dada zake Samuel.
iv) mwandishi pia anaonyesha kuwa wasichana wanafanya vizuri masomoni kuliko wavulana mf dada zake Samuel.
V Elimu inasisitiza sana kupita mtihani na mwanafunzi akianguka mtihani anaonekana ameanguka maishani. Mfano Samuel anaamua kujitia uhai.
Wazazi wao wa kiume matarajio makubwa sana katika elimu ndio waweze kuwatunza uzeeni.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:29


Next: X and Y are two variables such that Y is partly constant and partly varies inversely as the square of X. If Y = 3...
Previous: Define the term Organization

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions