“... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri” a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili. c)...

      

“... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili.
c) Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana ?
d) Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.

  

Answers


Kavungya
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
• haya ni maneno ya Mago
• anawaeleza wananchi wa Madongoporomoka
• wako katika mkahawa Mshenzi wa Mago
• wanajadili kuhusu namna ya kuzuia haki isiangamizwe

b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili.
• ana busara - anajua kupambana na wakubwa kunahitaji ushirikiano
• mwenye bidii - anajibidiisha kulinda haki na pia katika mkahawa wake
• mtetezi wa haki - anakataa mashamba yanyakuliwe anatafuta wakili mwaminifu
• mshawishi - anafaulu kuwahamasisha wanakijiji wote kujiandaa ili hukabiliana na wanyakuzi

c) Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana ?
• hali ya wanamadongoporomoka - wataenda wapi wakifurushwa
• umoja / ushirikiano baina ya makabwela
• maendeleo ya madongoporomoka
• mchango wa maskini katika kuendeleza nchi mbele

d) Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.
• umoja
• haki
• ushirikiano
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:33


Next: The table below shows the number of students who scored marks in mathematics test.
Previous: Define the term Administration.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions