
Tulipokutana Tena
• wazazi wa Bogoa - ni walezi wema ingawa ni maskini hawataki. Bogoa alelewe na wazazi wengine
o Mapenzi kifaurongo
• wazazi wa Penina Bw & Bi Kitane) wamewajibika katika kumlea Penina. Wanampa fedha za kutosha kila wiki
• licha ya kuwa maskini wazazi wa Dennis wanajizatiti sana kumpeleka chuoni hadi chuo kikuu
o Shoga yake Dada ana ndevu
• wazazi wake Safia na Lulua wanawapenda sana wanao
• wanawapeleka wanao shuleni na kuwapa safia nafasi ya kusoma pale nyumbani
• wazazi hawa pia wana mapuuza. Wanamwamini mwanao kupita kiasi
o Mama Bakari
• babake Sara ni mkali sana, Sara anapobakwa anaogopa kumwambia kuwa ana ujauzito
• baadaye anabadilika wa kuwa mpole, anamfariji
• mamake Sara ni dhaifu, hawezi kumsaidia Sara
o Ndoto ya Mashaka
• wazazi wa Samueli wanajinyima ili kuwasomesha watoto wao
• Babake Samueli aliuza ng’ombe wengi ili kumsomesha Samueli
• mamake Samueli anatumiwa kuonyesha mapenzi ya mzazi ni ya kudumu
• babake Samueli anatumiwa kuonyesha kukata tamaa / kutamauka
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:37