Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa” a. Eleza muktadha wa dondoo hili. b. Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili. c. Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili.

      

“…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili.
b. Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili.
c. Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili.

  

Answers


Kavungya
a. Eleza muktadha wa dondoo hili.
i. Ni kauli ya msimulizi wa hadithi.
ii. Inamrejelea Samueli, mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne.
iii. Samueli yuko katika faragha ya msalani pale shuleni alikoingia pasi na kusukumwa na haja.
iv. Hii ni baada ya kurushiwa ,matokeo na mwalimu mkuu na kuona kuwa amefeli mtihani.

b. Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili.
. Samueli ni;
i. Muoga - Anaonesha uoga anapoingia katika ofisi ya mwalimu mkuu na anapoingia nae anasitasita ishara ya kuwa muoga. Analemewa kuwakabili wazazi wake na kuwaeleza kuwa amefeli mtihani. Anatetemeka pia anapomuona baba yake pale bawani alipojitosa ili afe.
ii. Mwenye majigambo : Anajigamba kuwa ana hakika atapita mtihani na kumshtua mwalimu mkuu ambaye alionesha kutokuwa na imani naye. Anazi kujipata kwa kudai kuwa anaelewa kuwa yeye si mwerevu sana lakini huweza kupanga mambo yake na kile asomacho ndicho hutokea katika mtihani.
Anajitapa kwa mpenzi wake Nina kuwa yeye ni bingwa wa masomo.
iii. Muongo : Ana hadaa baba yake kuwa hakupata matokeo kwa kuwa hakuwa amekamilisha kulipa karo.
iv. Mwenye bidii : Anasema alikuwa akitembea mwendo wa kilomita 6 kuenda shuleni kila siku na kuwa alihudhuria madarasa yake vizuri.
v. Bwege : Kutokana na majibu ya yale ambayo anasema anayajua, anaonyesha kuwa zuzu na si ajabu alifeli mtihani.
vi. Mcheshi : Anachekesha kwa kauli yake kuhusu mwalimu mkuu na wazazi wake. Anasema kuhusu mwalimu mkuu, “ Labda mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu. Labda anataka kufanyiwa operesheni ya ubongo ama anahitaji maombi hasa atakuwa na akili razini tena” kuhusu wazazi wake anasema,
“….Mama na baba wameumbwa kwa aina tofauti za udongo”
vii. Mwepesi wa kukata tamaa : Kufeli mtihani shuleni anaona kana kwamba amefeli maishani. Hii ndio sababu anaamua kujiua.

c. Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili.
i. Anasumbuliwa na kufeli mtihani. Anaona juhudi zake nyingi za kutembea kilomita sita kuenda shuleni na kuwa na mahudhurio mazuri darasani zimeshindwa kuzaa matunda.
ii. Analemewa na vipi alivyofeli mtihani ilhali kuna mambo aliyoyajua na alihudhuria madarax vizuri.
iii. Anaona muda wa miaka mine, karo iliyolipwa na baba zimepotea.
iv. Anashindwa kama kuanguka mtihani ina maana kuwa hajui lolote.
v. Anaona kuwa baba yake hataelewa akimwambia kuwa amefeli mtihani.
vi. Anaona kama amesaliti wazazi wake, ilhali yeye kama mwana wa kiume wa pekee ndiye tegemeo lao la kuwakwamua katika lindi la uchochole
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:41


Next: Give the differences between administration and management.
Previous: a) PQRS is a quadrilateral with vertices p(1, 4) Q(2, 1), R(2, 3) and S(6, 4). On the grid provided plot the quadrilateral

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions