Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Alfa Chokocho : Tulipokutana tena “ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.” i) Eleza muktadha wa dondoo hili. ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira...

      

Alfa Chokocho : Tulipokutana tena
“ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii.
iii) Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”

  

Answers


Kavungya
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
i. Haya ni maneno ya Bogoa Bakari.
ii. Anawaambia mkewe Sakina, Sebu na mkewe Tunu, Kazu na mkewe Bi Tunu (ataje angalau wahusika wawili ndipo atuzwe)
iii. Wamo katika kilabu ya pogopogo.
iv. Bogoa anawasimulia hadithi kuhusu jinsi alivyotolewa nyumbani kwao na kupelekwa kwa Bi. Sinai aliyemtesa sana

ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii.
i. Kuchimuza suala la umaskini - Wazazi wake Bogoa hawana uwezo wa kununua sabuni / Bogoa na baba yake kutembea kwa miguu bila ya viatu hadi mjini.
ii. Kuonyesha masaibu ya wanakijiji - walikuwa na tatizo lamaji kwa maana yalikuwa
hayapatikani karibu. Walitembea masafari marefu kuyatafuta.
iii. Kumfumbulia Sebu fumbo alilotaka kufumbua - Amejua sababu ya Bogoa kutoroka nyumbani kwa Bi. Sinai.
iv. Kufichua aliyempeleka Bogoa kwa Bi. Sinai - baba yake.
v. Kusawiri maudhui ya mapenzi - mapenzi ya Bogoa kwa nduguze kwa wazazi wake yalimfanya kutotaka kutengana na familia yake.
vi. Kusisitiza kwamba Bogoa hakutaka kuishi na marafiki wa baba yake ingawa alisema kwamba ni watu wazuri– alilia na kupigwa ukwenzi.
vii. Kusawiri maudhui ya elimu - Baba yake Bogo anamwambia kwamba angepelekwa shuleni kusoma.
viii. Kuonyesha ukali wa baba yake Bogoa - Bogoa alipokataa kuenda kwa marafiki zake mjini alimtishia kumchapa.
ix. Kuendeleza maudhui ya ajira ya watoto - Bi. Sinai alimtumia Bogoa kufanya kazi ya nyumbani badala ya kumpeleka shuleni.
x. Kuonyesha swala la ukiukaji wa haki za watoto.-Bi. Sinai anamtumia Bogoa kufanya kazi za nyumbani badala ya kumpeleka shuleni.
xi. Kuonyesha maudhui ya utabaka - Bi Sinai anwaambia wanawe kwamba watoto wa maskini hawastahili kusoma, kazi yao ni kutumwa.
xii. Kufichua ukatili wa Bi.Sinai - Anamchoma Bogoa baada ya kulala na kuacha mandazi kuungua.
xiii. Kuonyesha maudhui ya uwajibikaji - Wazazi wake Bogoa walimtembelea ili kumjulia hali.
xiv. Kuonyesha udanganyifu wa Bogoa - Bogoa anachomwa na Bi. Sinai lakini anamwambia Sebu aliungua akiepua maji moto.
xv. Kuendeleza maudhui ya Siri - Bogoa aliteseka sana mikononi mwa Bi. Sinai ila hakuwahi kumwambia rafikiye Sebu.
xvi. Kubainisha masaibu ya Bogoa - Bi. Sinai hakumruhusu kutangamana na wazazi wake walipomtembelea, alikula makombo, anatusiwa, anasumbuliwa, anakatazwa kucheza na watoto wengine.

iii) Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”
. Mashaka ni mambo magumu yanayomfika mtu katika maisha. Jina hili linamwafiki kwani ;
i. Wazazi wake wote walikufa mara tu baada ya kuzaliwa hivyo kuyakosa malezi yao.
ii. Mlezi wake Biti Kidebe anaugua miguu; hivyo inambidi amuugize ilhali yu mdogo kiumri.
iii. Anaanza kufanya vijikazi vya kuchuma karafuu na kuangua nazi akiwa mdogo kiumri ili kutafuta kipato cha kujilisha na mlezi wake Biti Kidebe.
iv. Alisoma akamaliza chumba cha nane kwa taabu na mashaka.
v. Mlezi wake, Biti Kidebe alikufa mara tu baada ya kumaliza masomo yake.
vi. Anafungishwa ndoa kwa lazima. Babake Waridi, mzee Rubeya anafika walimokuwa akiwa na watu wanne na kumfungisha ndoa bila ya yeye kuwa na habari.
vii. Familia nzima ya mzee Rubeya (babake Waridi) ilikosa raha kwa sababu ya mwanao Waridi kuolewa na yeye ambaye ni maskini . Waliaibikia ndoa hii hadi wakahamia Yemeni.
viii. Anaishi maisha ya kimaskini kule Tandale. Inambidi kufanya kazi ya ulinzi usiku ili kuilisha aila yake. Anaishi kwenye nyumba yenye paa linalovuja.
ix. Mkewe Waridi anamtoroka kwa sababu ya umaskini.
x. Hana kiti, meza, kitanda wala godoro katika makazi yake.
xi. Anafanya kazi ila mshahara anaolipwa ni wa mkia wa mbuzi, yaani mshahara duni.
xii. Ana watoto wengi hadi hawana nafasi ya kulala kwenye chumba chake cha kupanga. Imebidi kumrai jiraniye kumkubalia wanawe wa kiume kulala jikoni mwake.
xiii. Hali ya mkewe Waridi kutoroka na wanawe kinamsababishia unyonge na unyong’onyevu
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:45


Next: Discuss the levels of management.
Previous: Give the differences between leadership and management.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions