‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’ Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba

      

‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’
Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba

  

Answers


Kavungya
a) Jitu linamaliza chakula chote kwenye Mkahawa Mshenzi bila kuwajali wateja waliokuwa pale.
b) Vibanda vya Wanamadongoporomoka vinabomolewa bila kujali watapokwenda wenye vibanda.
c) Wakubwa wanaweka vikwazo katika sheria kwa makusudi ili kuwazuia watu wadogo kutetea mali zao.
d) Wanamadongoporomoka hawahusishwi katika mipango ya maendeleo katika eneo lao.
e) Askari wa baraza la mji na jeshi la polisi wanatumiwa kuwafurusha Wanamadongo wenye njaa katika makazi yao badala ya kuwahakikishia usalama wao.
f) Majengo mengi yanajengwa katikati ya jiji kiwango cha mtu kukosa nafasi ya kuvuta pumzi.
g) Wanasheria kukosa kuwa waaminifu wanapokabiliwa na sheria ngumu.’’siku wanasheria waaminifu ni adimu kama haki yenyewe!’’
h) Wakubwa wanataka kunyakua ardhi ya wasiokuwa na nguvu kwa lazima baada ya
i) Wakubwa wanataka kuwahonga kwa visenti vyao vichache ili waondoke ilhali hawana pa kwenda.
j) Mazingira chafu- Madongoporomoka ndiko kunako pachapacha za kila kitu;tope na uchafu unaonyekenya,makaro na uvundo unaopasua mianzi ya pua.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:51


Next: Discuss the traditional approach theory of leadership and management.
Previous: Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions