Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.

      

Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.

  

Answers


Kavungya
a) Ubinafsi- Kuna ubinafsi na ulafi katika jamii ya kisasa kama ilivyo katika hadithi.Jitu linamaliza chakula chote kwenye Mkahawa Mshenzi bila kuwajali wateja wengine.
b) Unyakuzi- Wakubwa wanataka kunyakua ardhi ya watu wadogo kama ilivyo katika jamii ya leo ambapo viongozi hunyakua ardhi ya watu maskini.
c) Dhuluma- Wananchi hukandamizwa kwa kubomolewa vibanda/makazi yao hata bila ilani na kuachwa wakihangaika jinsi ambavyo inafanyikia Wanamadongoporomoka.
d) Ufisadi- Wakubwa wanataka kuwahonga na vijisenti vidogo ili wahame makazi yao jinsi viongozi katika jamii ya leo huwahonga wananchi maskini na kunyakua mali yao.
e) Sheria zenye vikwazo- Katika jamii ya leo,sheria huwapendelea matajiri na viongozi kwani wao huweka vikwazo makusudi ili kuwazuia maskini na wasio na nguvu kutetea haki zao.Hali ni hiyo hiyo katika hadithi ya Tumbo Lisiloshiba.
f) Kutengwa- Wananchi hawahusishwi Na viongozi kikamilifu katika mipango ya maendeleo ya maeneo yao.Wanamadongoporomoka hawahusishwi katika mipango ya maendeleo.
g) Mazingira chafu- Hali katika mtaa wa Madongoporomoka ni mbaya,viongozi hawasafishi mtaa wao,kama ilivyo katika mitaa duni nyingi katika jamii ya leo.
h) Wanasheria wasio waadilifu- Jinsi inavyokuwa vigumu kupata wanasheria waadilifu katika jamii ya leo, ndivyo ilivyokuwa adimu kuwapata wanasheria waaminifu kama haki yenyewe katika jamii ya hadithi ya Tumbo Lisiloshiba.
i) Msongamano mijini- Jiji lilikuwa limejaa limejaa kila mahali;mall,majumba ya muziki,maduka makuu,shule, vyuo,hospitali,mahakama,majumba ya ofisi,n.k. Jinsi ilivyo katika miji mikuu mingi leo.
j) Matumizi mabaya ya vyombo vya dola- Askari wa baraza la mji na jeshi la polisi walitumiwa kuwafurusha wanamadongoporomoka badala ya kuwahakikishia usalama wao,Vyombo vya dola vinatumiwa vibaya na viongozi wa sasa.
k) Maendeleo- Kuna maendeleo yaliyopiga kasi katika jamii ya sasa kama ilivyo katika jamii ya hadithini.Jiji limejaa majumba ya mikahawa,malls,deparmental stores,casinos,n.k.
l) Ushirikiano- Kuna ushirikiano na umoja wa wananchi wanaonyanyaswa katika jamii ya sasa jinsi Mzee Mago alivyowakusanya wanamadongoporomoka ili kutetea haki zao.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:53


Next: ‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’ Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba
Previous: Discuss the human relations approach.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions