“Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”…. (a) Eleza muktadha wa dondoo hili (b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (c) Eleza...

      

“Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
(c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya.
(d) Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.
Taja mambo sita

  

Answers


Kavungya
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili
• Maneno yalisemwa na mwenye tumbo lisiloshiba
• Anamwambia mzee Mago.
• Wako kwenye hoteli ya mzee Mago.
• Alikuwa amemaliza kula na alikuwa akidokeza kuwa keshoye angefika pale

(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
• Takriri – Kama … kama
• Mdokezo . salama …..
• Kisengere mbele/ mbinu elekezi
• Kama tutafungua milango ya nyumba zetu.

(c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya.
• Mlafi – anakula chakula chote kwenye mkahawa.
• Mwenye tamaa – anatamani ardhi ya madongoporomoka.
• Mdunishaji – Maslahi ya wengine hawajali wanamadongoporomoka watahamia wapi.
• Mwenye upeo mfupi – Hakufikiria kuwa wanamadongoporomoka wangeweza kupingana naye na kukatia hapo.
• Mwenye dharau – Anamtamkia mzee Mago kwa ujeuri na kusema ‘Nimekuahidi kuja kula ardhi yako hii leo’.
• Mkakamavu- hakujali kama watu wangemvamia alipokuwa akila chakula chote kwa mabavu huko kwa mzee Mago

(d) Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.
Taja mambo sita
I) Ufisadi – Matajiri wamenyakua mali ya umma.
(ii) Unyakuzi wa ardhi – mwenye tumbo lisiloshiba anataka kunyakua mashamba ya anamadongoporomoka.
(iii) Nyakanyaka za nyumba – Nyumba nyingi sana zimejengwa kila mahali jijini.
(iv) Matumizi mabaya ya vyombo vya dola – askari wanatumiwa kawalinda mabwanyenye wanaonyakua ardhi.
(v) Ubomoaji wa vibanda – vibanda vya kina yahe vinabomolewa huko madongoporomoka.
(vi) Utabaka - Kuna matajiri na maskini. Matajiri wanaishi jijini nao maskini wanaishi madongoporomoka.
(viii) Maandamano – maskini wanahitajitetea kwa kuandaa maandamano
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:58


Next: The position of two towns P and Q are given to the nearest degrees as P(45oN, 110oW) and Q (45oN, 70oE) Take ??=3.142, Radius of...
Previous: Compete the table below

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions