Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa kitanzi. a)Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo. b)Jadili vipengele...

      

Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa kitanzi.
a)Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo.
b)Jadili vipengele vitano vya sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima.
c)Onyesha dhiki iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo.

  

Answers


Kavungya
a)Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo.
Tashbihi - kama vile katia saini . . .
Msemo - kujitia kitanzi

b)Jadili vipengele vitano vya sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima.
• lazima angeendelea kufanya kazi ya umetroni.
• lazima kazi ya upishi walifaa kuifanya wote wawili.
• lazima wangepata mtoto mmoja pekee.
• lazima Dadi angetakiwa kunadhifisha nyumba na kifua nguo.
• lazima angekuwa na uhuru wa kuvalia kisasa.
• lazima angekuwa na uhuru wa kutangamana na wanaume wengine

c)Onyesha dhiki iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo.
• Alimshuku mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.
• Aliijihisi mtumwa katika ndoa yake.
• Alikejeliwa na kusimangwa na majirani.
• Alianguka na kuumia vibaya alipoenda kumchunguza mkewe kwa kukisia alikuwa na uhusiano na mwalimu mkuu.
• Alitawaliwa na chuki dhidi ya mkewe.
• Alikosa raha hata kushindwa kukila chakula alichoandaliwa.
• Hakuwa na muda wa kupumzika
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:07


Next: Give the requirements for registration of board of management.
Previous: Evaluate the following;

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions