Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

‘’Acha nijiondelee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe.” a) Eleza muktadha wa dondoo hili b) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili. c) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika...

      

‘’Acha nijiondelee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili.
c) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika hadithi hii.

  

Answers


Kavungya
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
• Haya ni mawazo ya Samueli.
• Ni baada ya baba yake kwenda shule ya upili ya Busukalale kushauriana na mwalimu mkuu kuhusu karo.
• Alikuwa karibu na bwawa lililopo kwenye kinamasi karibu na kwao
• Alitaka kujitosa majini afe

b) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili.
Samueli
• Alikuwa mwanfunzi wa shule ya upili ya Bukukalala – kwa muda wa miaka minne
• Ni Mcheshi
• Anasema, ‘Labda mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu.’
• Pia anasema kuwa babake na mamake wameumbwa kwa aina fulani ya udongo.
• Ni mwongo / laghai
• Alidanganya babake kuwa hakupata matokeo ya mtihani kwa sababu hakuwa amemaliza kulipa karo.
• Ni mwoga
• Anaogopa anapoingia ofisi ya mwalimu mkuu na anasitasita anapozungumza.
• Ana machoka na ndiyo maana akapewa jina Rasta shuleni
• Huvunjika moyo upesi.
• Kutofaulu mtihani anakuona kama ni kuwaletea wazazi wake aibu.
• Anaamua kijitosa majini ili afe.
• Hakuna maana ya kuendelea kuishi
• Ana majivuno
• Anaelewa kuwa yeye si mwerevu lakini anajua kupanga mikakati na anaamini ana bahati kama mtende.
• Anaamini amepita mtihani vizuri na matokeo yake yangemshtua mwalimu mkuu kwa sababu hakuwa na imani naye.
• Baba yake anamgombeza na kuona hafai.
• mama yake anamtia moyo kwa kumwambia kuwa hajafeli mtihani wa maisha.

c) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika hadithi hii.
• Kinaya
• Ni kinaya Samueli kupoteza miaka minne ya kwenda shule bila mafanikio.
• Samueli anamdanganya baba yake ili atembee kilomita sita kutafuta matokeo ya mtihani ilhali alikuwa amepewa matokeo yake.
• Tashhisi/ uhuishi
• Nzi wa kijani wa samawati waliokula wakashiba
• Linampokea kwa vilio nao mnuko kwa kughasi unapokea kwa vigemo.
• safu safi ya D na E ilimkondolea macho bila kupesapesa.
• Alimpa jicho safu ya maji akaona yanasumbuka na kuhangaika.
• SADFA
• - Ilisadifu kuwa siku na wakati ambapo Samueli alitoka kujirusha majini ili afe, Siku hiyo ilikuwa tofauti kwani wachunga walipitia hapo wakiwapeleka mifugo malishoni hawakuwapo hivyo ikawa rahisi kujitosa majini.
• baada ya Samueli kujitosa majini na kupiga mikupuo kadhaa ya maji, mwanaume mmoja akawa ameachwa na basi na akaamua kutumia njia karibu na kumwokoa Samueli.
• Taharuki
• Kuna wanafunzi waliotokea ofisini mwa mwalimu mkuu wakiwa na furaha na huku machozi yanawatoka.
• Nina alimwacha Samueli kutokana na vituko vyake au la!
• Maisha ya Samuel yaliendelea Aje?
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:16


Next: In a Chemistry experiment, a boy mixed some acid solution of 45% concentration with an acid solution of 25% concentration. In what proportion should the...
Previous: (a) Find the greatest common divisor of the term 9x3y2 and 4xy4.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions