Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
• Haya ni mawazo ya Samueli.
• Ni baada ya baba yake kwenda shule ya upili ya Busukalale kushauriana na mwalimu mkuu kuhusu karo.
• Alikuwa karibu na bwawa lililopo kwenye kinamasi karibu na kwao
• Alitaka kujitosa majini afe
b) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili.
Samueli
• Alikuwa mwanfunzi wa shule ya upili ya Bukukalala – kwa muda wa miaka minne
• Ni Mcheshi
• Anasema, ‘Labda mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu.’
• Pia anasema kuwa babake na mamake wameumbwa kwa aina fulani ya udongo.
• Ni mwongo / laghai
• Alidanganya babake kuwa hakupata matokeo ya mtihani kwa sababu hakuwa amemaliza kulipa karo.
• Ni mwoga
• Anaogopa anapoingia ofisi ya mwalimu mkuu na anasitasita anapozungumza.
• Ana machoka na ndiyo maana akapewa jina Rasta shuleni
• Huvunjika moyo upesi.
• Kutofaulu mtihani anakuona kama ni kuwaletea wazazi wake aibu.
• Anaamua kijitosa majini ili afe.
• Hakuna maana ya kuendelea kuishi
• Ana majivuno
• Anaelewa kuwa yeye si mwerevu lakini anajua kupanga mikakati na anaamini ana bahati kama mtende.
• Anaamini amepita mtihani vizuri na matokeo yake yangemshtua mwalimu mkuu kwa sababu hakuwa na imani naye.
• Baba yake anamgombeza na kuona hafai.
• mama yake anamtia moyo kwa kumwambia kuwa hajafeli mtihani wa maisha.
c) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika hadithi hii.
• Kinaya
• Ni kinaya Samueli kupoteza miaka minne ya kwenda shule bila mafanikio.
• Samueli anamdanganya baba yake ili atembee kilomita sita kutafuta matokeo ya mtihani ilhali alikuwa amepewa matokeo yake.
• Tashhisi/ uhuishi
• Nzi wa kijani wa samawati waliokula wakashiba
• Linampokea kwa vilio nao mnuko kwa kughasi unapokea kwa vigemo.
• safu safi ya D na E ilimkondolea macho bila kupesapesa.
• Alimpa jicho safu ya maji akaona yanasumbuka na kuhangaika.
• SADFA
• - Ilisadifu kuwa siku na wakati ambapo Samueli alitoka kujirusha majini ili afe, Siku hiyo ilikuwa tofauti kwani wachunga walipitia hapo wakiwapeleka mifugo malishoni hawakuwapo hivyo ikawa rahisi kujitosa majini.
• baada ya Samueli kujitosa majini na kupiga mikupuo kadhaa ya maji, mwanaume mmoja akawa ameachwa na basi na akaamua kutumia njia karibu na kumwokoa Samueli.
• Taharuki
• Kuna wanafunzi waliotokea ofisini mwa mwalimu mkuu wakiwa na furaha na huku machozi yanawatoka.
• Nina alimwacha Samueli kutokana na vituko vyake au la!
• Maisha ya Samuel yaliendelea Aje?
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:16
- ‘Shogake dada ana ndevu’ Safia
Eleza sifa za wahusika wafuatao.
i) Mwalimu Musi
ii) Jairo
iii) Sera
iv) Mke wa Jairo(Solved)
‘Shogake dada ana ndevu’ Safia
Eleza sifa za wahusika wafuatao.
i) Mwalimu Musi
ii) Jairo
iii) Sera
iv) Mke wa Jairo
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Huku ukirejelea diwani ya Tumbo lisiloshiba fafanua matatizo yanayokumba vijana katika jamii(Solved)
Huku ukirejelea diwani ya Tumbo lisiloshiba fafanua matatizo yanayokumba vijana katika jamii
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa kitanzi.
a)Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo.
b)Jadili vipengele...(Solved)
Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa kitanzi.
a)Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo.
b)Jadili vipengele vitano vya sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima.
c)Onyesha dhiki iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Kwa kuzingatia hadithi zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza katika tumbo lisiloshiba (Diwani)(Solved)
Kwa kuzingatia hadithi zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza katika tumbo lisiloshiba (Diwani)
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “Kesho panapo majaaliwa. Kesho kama sote tutaamka…….. kama tutafungua milango ya nyumba zetu zinazosimamia juu ya ardhi hii adhimu…”
a Eleza muktadha wa dondoo hili
b Eleza...(Solved)
“Kesho panapo majaaliwa. Kesho kama sote tutaamka…….. kama tutafungua milango ya nyumba zetu zinazosimamia juu ya ardhi hii adhimu…”
a Eleza muktadha wa dondoo hili
b Eleza sifa nne za msemaji
c) Taja mbinu zozote mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili
d Kwa kurejelea hadithi nzima onyesha namna jamii ya kisasa ina tumbo lisiloshiba
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Ukengeushi huzorotesha maendeleo ya kijamii. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya ‘Mkubwa’.(Solved)
Ukengeushi huzorotesha maendeleo ya kijamii. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya ‘Mkubwa’.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
(c) Eleza...(Solved)
“Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
(c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya.
(d) Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.
Taja mambo sita
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.(Solved)
Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- ‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’
Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba(Solved)
‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’
Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Sekta ya elimu ina changamoto nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo :
a) Mapenzi ya Kifaurongo
b) Shogake dada ana Ndevu
c) Mwalimu Mstaafu
d) Mtihani wa maisha
(Solved)
Sekta ya elimu ina changamoto nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo :
a) Mapenzi ya Kifaurongo
b) Shogake dada ana Ndevu
c) Mwalimu Mstaafu
d) Mtihani wa maisha
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Alfa Chokocho : Tulipokutana tena
“ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira...(Solved)
Alfa Chokocho : Tulipokutana tena
“ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii.
iii) Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili.
b. Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili.
c. Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili.(Solved)
“…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili.
b. Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili.
c. Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi.(Solved)
Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili.
c)...(Solved)
“... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili.
c) Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana ?
d) Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Jadili maudhui ya elimu katika Diwani ya Tumbo lisiloshima ukizingatia hadithi zifuatazo:
a) Mapenzi ya kifaurongo
b) Shagake dada ana ndevu.
c) Mamake Bakari .
d) Mwalimu mstaafu.
e) Mtihani...(Solved)
Jadili maudhui ya elimu katika Diwani ya Tumbo lisiloshima ukizingatia hadithi zifuatazo:
a) Mapenzi ya kifaurongo
b) Shagake dada ana ndevu.
c) Mamake Bakari .
d) Mwalimu mstaafu.
e) Mtihani wa maisha.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “Hapana cha ala, bwana. Liswmwalo lipo,kama halipo linakuja. Kumbuka msemo mabrafu wa siri ya kata iulize mtungu . Mtungi wenyewe ni mimi ……”
a) Eleza muktadha...(Solved)
“Hapana cha ala, bwana. Liswmwalo lipo,kama halipo linakuja. Kumbuka msemo mabrafu wa siri ya kata iulize mtungu . Mtungi wenyewe ni mimi ……”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha tamathali mbili za lugha zilitotumiwa katika dondoo hili
c) Fafanua sifa moja ya msemaji inayodokezwa na dondoo hili
d) Msemaji wa mabo haya baadaye anageuka kata na kupiga mbizi mtungini. Eleza ukitoa mfano kutoka hadithi.
e) Eleza maudhui ya malezi kama yanavyojotokeza katika hadithi ya shogaka Dada ana Ndevu .
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tunakula”
(a) Eleza mukadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika.
(c) Eleza umuhimu wa mnenaji.
(d) “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza”...(Solved)
“Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tunakula”
(a) Eleza mukadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika.
(c) Eleza umuhimu wa mnenaji.
(d) “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza” Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli hii.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “Hebu sikiza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Taja na utoe mifano ya mbinu nne za lugha zilizotumika katika...(Solved)
“Hebu sikiza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Taja na utoe mifano ya mbinu nne za lugha zilizotumika katika dondoo
c) Onyesha ukweli wa kauli “ nzi kufia kidondani” unavyodhihirishwa na wahusika katika hadithi.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “ Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.” Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano.(Solved)
“ Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.” Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “… Ningeondoka shuleni mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.”
a) Eleza muktadha wa maneno haya
b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza
c) “ Kinaya kimetumika...(Solved)
“… Ningeondoka shuleni mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.”
a) Eleza muktadha wa maneno haya
b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza
c) “ Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu.” Thibitisha
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)