Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kwa kurejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na ya Mapenzi ya Kifaurongo, fafanua maudhui ya utabaka.

      

Kwa kurejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na ya Mapenzi ya Kifaurongo, fafanua maudhui ya utabaka.

  

Answers


Kavungya
Utabaka – Tumbo Lisiloshiba
• Kuna tabaka la mabwenyenye(jitu) na lile la wanyonge(wakazi wa madongoporomoka).
• Tabaka la mabwenyenye linaendesha dhuluma dhidi ya wanyonge k.m jitu kubwa linasimamia ubomoaji wa vibanda vya wakazi wa Madongoporomoka.
• Tabaka la mabwenyenye linatumia vyombo vya dola kama askari wa baraza la mji na askari polisi kuwakandamiza wanyonge.
• Ardhi ya wakazi/watu wa madongoporomoka inatwaliwa na mabwenyenye.
• Wana sheria wamezibwa midomo kwa fedha za mabwenyenye.
• Tumbo lisiloshiba linaashiria wenye mamlaka ambao hawatosheki na wanataka kunyakua kile kidogo walichonacho wanyonge.

Utabaka – Mapenzi ya Kifaurongo
• Wazazi wa Dennis Walikuwa wachochote na hawakuwa na mali yoyote.
• Dennis alikuwa mwanachuo wa tabaka la chini. Umaskini uliostakimu kwao hauna mfano.
• Kila asubuhi waamkapo, mipini ya majembe huwa mabegani mwa wazazi wa Dennis kutafuta kibarua cha kuwalimia matajiri mashamba.
• Dennis anayamezea mate magari makubwa makubwa ya watu wenye nacho.
• Dennis alihizika akiwa chuoni kutokana na umaskini wake anapowatazama wanafunzi wenzake walivyonenepa na kuwanda. Mavazi yao ni laini kutoka Uingereza, Ujerumani,Marekani, na Ufaransa.
• Wanafunzi wa tabaka la juu wana simu za thamani, wengine wanabeba vipakatatahishi na ipad.
• Wanafunzi hao walisomea shule za upili za hadhi kubwa – za mikoa au za kitaifa.
• Kutazamia shule za vijijini kumwibua huigwa katika mitihani ya kitaifa ni kama kutarajia kupata maziwa kutoka kwa kuku.
• Mavazi ya Dennis ni duni, kula kwa shida . n.k
• Wenye jadi kubeli wanapita juu na wachochote wanapita chini ingawa wamo katika chuo kimoja na wanafanya masomo mamoja.
• Penina kumsikitikia Dennis kutokana na hali yake duni ya ufukara.
• Tofauti ya matabaka iliwatia kiwewe wazazi wa Dennis na wale wa penina.
• Penina kusema kuwa hawezi kuolewa na mwanamume asiye na kazi yenye mshahara mkubwa.
• Shakila alikuwa na tabaka la juu. Mama yake alikuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la uchapishaji.
• Ukosefu wa ajira unamfanya Dennis afukuzwe na penina.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:18


Next: (a) Find the greatest common divisor of the term 9x3y2 and 4xy4.
Previous: Anwani ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni mwafaka kwa hadithi hii. Fafanua

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions