Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Huku ukirejelea hadithi za: i) Mapenzi ya kifaurongo ii) Shogake dada ana ndevu iii) Mame Bakari Fafanua maudhui ya mapenzi kama yanavyosawiriwa.

      

Huku ukirejelea hadithi za:
i) Mapenzi ya kifaurongo
ii) Shogake dada ana ndevu
iii) Mame Bakari
Fafanua maudhui ya mapenzi kama yanavyosawiriwa.

  

Answers


Kavungya
i) Mapenzi ya kifaurongo
- Dennis anampenda Penina kwa dhati.
- Anamtambulisha kwa wazazi wake.
- Anatazamia kumuoa haswa pindi atakapopata kazi.
- Wazazi wa Dennis wana mapenzi kwa mwanao k.m wanajitahidi kufanya vibarua vya kuwalimia matajiri mashamba ili wakimu mahitaji yake.
- Wazazi wa Penina wanampenda kwa dhati wanakimu mahitaji yake chuoni k.m pesa matumizi elfu tano kila wiki, wanamlipia kodi ya nyumba.
- Mamake Shakila anamtafutia mwanaye kazi katika shirika la uchapishaji.
- Mapenzi ya Penina kwa Dennis si ya dhati. Licha ya wao kuishi pamoja anasema kuwa hawezi akaolewa na mtu asiye na mali.
- Dennis anapokosa kazi Penina anamfurusha.
- Anamdharau na kumnyima chakula kwa sababu hakuchangia chochote kununua chakula.
- Wanafunzi wa chuo cha kivukoni wanaonekana wengi wao kuwa na mahusiano ya kimapenzi k.m huonekana wakiongozana mvulana na msichana kufanya starehe za hapa na pale.
- Mapenzi kati ya Penina na mpenzi wa awali ambaye alikuwa wa tabaka la juu na wakafarakana.

ii) Shogake dada ana ndevu
mapenzi ya dhati
- -pana mapenzi ya dhati kati ya bwana Masudi na Bi Hamida – wanazungumza mambo mazito nay a ndani kila jioni wakisubiri usingizi uwachukue.
- Bwana Masudi na Bi. Hamida wanampenda binti yao. Upendo huu unadhihirika kwa nama ambavyo wanamlea kwa makini.
- Wanahakikisha binti amekuzwa kwa maadili mema.
- Bwana Masudi na Bi. Hamida wanadhamini masomo kwani wanampa binti yao msaada unaohusiana na masomo kadri ya uwezo wao.
- Ndugu yake Sofia alionyesha mapenzi kwa dadake, anapomweleza mama jinsi yeye na rafikiye anavyocheza.
Mapenzi ya uongo
- Mapenzi kati ya Sofia na Kimwana ni ya uongo – Sofia anaposhika mimba wanajaribu kuavya jambo ambalo linasababisha kifo chake.

iii) Mame Bakari
mapenzi ya dhati.
- Wazazi wa Sara walimpenda kwa dhati – kwani hata baada ya wao kujua kuwa ni mja mzito hawakumfokea.
- Anapojifungua wazazi wake wanampokea vyema.
Pana mapenzi ya dhati kati ya Sara, Beluwa na Sarina. Baada ya Sara kuwaeleza yaliyomfika walimsaidia
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:25


Next: Mutai imports rice from the United States at initial cost of 500 US Dollars per tonne. He then pays 20% of this amount as shipping costs...
Previous: Given that tan x =5/13,find the value of the following without using mathematics tables or a calculator:

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions