Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika ‘Tumbo lisiloshiba na Hadithi nyingine’, fafanua maudhui ya utabaka.

      

Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika ‘Tumbo lisiloshiba na Hadithi nyingine’, fafanua maudhui ya utabaka.

  

Answers


Kavungya
a)Tumbo Lisiloshiba
Utabaka.
-Kuna tabaka la mabwanyenye na tabaka la wanyonge. Tabaka la mabwanyenye linaendesha dhuluma dhidi ya wanyonge. Katika hadithi, hii jitu kubwa linaonekana likisimamia shughuli ya ubomoaji wa vibanda vya wakazi wa Madongoporornoka. Tabaka hilo la mabwenyenye linatumia vyombo vya dola kama askari wa baraza la mji na askari polisi katika kuwakandamiza wanyonge.

b) Mmapenzi Va Kifaurongo
Utabaka,
• Dennis anatoka katika familia maskini, Wazazi wake walikua wachochole hawakua na mali yoyote. Walijitahidi sana kutoka katika ufukwe huo haikuwezekana. .
• Dennis alikuwa mwanachuo wa tabaka la chini. Kulikuwa na wengine ambao walikua na fedha tele. Wazazi wao walimiliki majumba mengi na wengine walikuwa na misururu ya mabasi na matatu ya abiria,
• Shakifa afikuwa wa tabaka lajuu. Mama yake alikuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la uchapishaji.
• Wanachuo waliotoka tabaka la juu walikua na maisha mazuri, libasi zao ni bora, wana simu nzuri, tarakilishi na vitu vingine. Dennis mavazi yake yalikua duni, kula kwa shida na kadhalika.
• Kulikuwa na watu walioendesha magari ya kifahari makubwa na mazuri.
• Wazazi wa Dennis ni wa tabaka la chini. Walifahamu kuweka majembe begani na kulima vibarua tu.

c) Ndoto Mashaka
Utabaka
• Kuna watu wengi maskini. Ingawaje wanajaribu kupigana nao, bado hawajawahi kujinasua. Mwandishi anaonyesha kuwa katika mtaa wake, wamo rnaskini wengi. Na si humo tu, kuna sehemu nyingi nyinginezo. Watu wa tabaka la chini wanakaa sehemu zisizo na mpangilio maalum wa ujenzi.
• Chumba cha Mashaka kwa mfano, kimepakana na choo cha jirani. Maji ya kuogea yanapita karibu na churnba chao.Watu wanaoishi katika mandhari haya ni wengi. Mvua ikinyesha kundi zima hili huwa rnashakani. Viongozi hutangaza kuwa watu wa bondeni wahame lakini hawapewi mahala badala.
• Tabaka la chini hubaguliwa. Mzee Rubeya anahamia na kurudi Yemeni maana
hakuweza kustahimili aibu ya binti yake kuolewa na mchochole.

d) Kidege
Utabaka.
• Kuna tabaka la midege mikubwa. Hii ina nguvu na midomo yao ni kama mapanga.
• Midege mikubwa inavamia na kutwaa visamaki vilivyokuwa katika kidimbwi cha bustani ya llala.
• Tabaka hili la midege mikubwa linaashiria tabaka la matajiri;watu wenye nguvu za kiuchumi katika jamii. Watu hawa hutumia nguvu zao kuwadhulumu wanyonge rasilimali na haki zao.
• Tabaka hili la videnge vidogo linaungana na kupambana dhidi ya uvamizi wa midege. Hatimaye videge vinashinda na kuifukuza midege mikubwa.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:28


Next: Given that tan x =5/13,find the value of the following without using mathematics tables or a calculator:
Previous: A solid consists of three discs each of 1.5cm thick with diameter of 4cm, 6cm and 8cm respectively. A central hole 2cm in a diameter is...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions