Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii” a) Eleza muktadha wa dondoo hili b) Taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili c)...

      

Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili
c) Fafanua sifa za msemaji
d) Jadili maudhui ya utabaka ukjirejelea hadithi husika.

  

Answers


Kavungya
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
msemaji ni dennis akimwambia Penina wakiwa chumbani mwa Dennis katika chuo. Penina alikuwa anamwelezea Dennis kuwa angetaka awe mpenzi wake ndipo Dennis anapinga kwani wanatoka matabaka tofauti

b) Taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili
msemo- tunapigania mikono ilekee vinywani
methali – mzoea vya sahani vya vigae hawezi

c) Fafanua sifa za msemaji
sifa za Dennis
- Msomi
- Mwenye bidii
- Mwepesi wa kushawishika
- Mwenye majuto
- Mwenye wasiwasi
- Limbukani wa mapenzi
- Mpweke

d) Jadili maudhui ya utabaka ukjirejelea hadithi husika.
o Matajiri wanaendesha magari ya kifahari
o Wazazi wa Dennis ni maskini
o Wazazi wa Dennis wanafanya kazi ya vibarua
o Dennis alikosa chakula aklanbywa uji
o Penina alitumiwa shilingi 5000 kila wiki za matumizi
o Wazazi wa wanafunzi wengfine walimiliki mabasi na matatu hivyo ni matajiri
o Wengine walimiliki nyumba za ghorofa
o Wanafunzi wengine walimiliki simu za dhamani
o Wengine walivalia mavazi ya vitambaa vya dhamani na vilivyovuytia
o Watato wa maskini hawakufanya vyema katika mitihani yao
o Dennis alikuwa bila mpenzi kwani vijanamaskini hawakupendwa
o Mpenzi wa zamani wa Penina alitoka kwenye aila yenye nafasi
o Shakila alitoka kwenye familia tajiri ambapo wazaziwe walimiliki shirika la uchapishaji
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:40


Next: Solve the simultaneous inequality below.
Previous: Find the value of m and n in the figure below.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions