“ Naapa na mola wangu sitofanya tena biashara hii.” a. Eleza muktadha wa dondoo hili b. Tathmini umuhimu wa mzungumzaji c. “Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa...

      

“ Naapa na mola wangu sitofanya tena biashara hii.”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
b. Tathmini umuhimu wa mzungumzaji
c. “Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa jamii.” Huku ukirejelea hadithi hii,thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi.

  

Answers


Kavungya
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
i.Haya ni maneno ya Mkumbukwa
ii.Anamwambia Mkubwa
iii.Wamo nyumbani mwa Mkumbubwa
iv.Ni baada ya kubadili nia na kutotaka kutumiwa na Mkubwa kusambaza unga/dawa za
kulevya kwa mateja

b. Tathmini umuhimu wa mzungumzaji
Mzungumzaji ni Mkumbukwa.Ana umuhimu ufuatao;
i.Ni kielelezo cha ufisadi.Anawahonga raia ili wamchague Mkubwa katika uchaguzi mkuu
ii.Anaonyesha maana ya methali ‘muui huwa mwema’.Amekuwa akitumiwa na Mkubwa kuuza unga lakini amebadilika na kumsuta Mkubwa kwa kuendesha biashara hiyo
iii.Ametumiwa kufichua masaibu ya mahabusu gerezani .Anaeleza jinsi wanavyolala sakafuni na chakula chao kuliwa na askari
iv.Ni kiwakilishi cha madhara ya kuuza unga.Anatiwa mbaroni na kufungwa kwa siku tatu baada ya kupatikana na furushi na bangi.
v.Ni mfano wa raia wanaondeleza uongozi mbaya .Anawahonga raia kumchagua Mkubwa aliye na kisomo duni na asiyestahili na kumwacha profesa.
vi.Ametumiwa kuufichua unafiki wa Mkubwa . Anamsuta Mkubwa kwa kufungua nyumba za kurekebisha tabia za vijana mateja ilhali ndiye anayewauzia unga.

c. “Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa jamii.” Huku ukirejelea hadithi hii,thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi.
Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari hasi kwa jamii.’’ Huku ukirejelea hadithi
hii,thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi.
i.Kufungwa – Mkumbukwa anatiwa mbaroni na kufungwa kwa siku tatu baada ya kupatikana na begi la unga
ii.Kusinzia – Mkumbubwa anadai kwamba vijana wanaotumia unga wanasinzia saa zote;hivyo kuishia kutofanya kazi.
iii.Vifo – Mkumbukwa anadai kwamba vijana wengi wamekufa kutokana na matumizi ya unga.
iv.Ufisadi – Biashara ya unga iliendeleza ufisadi katika jamii,Mkubwa anamhonga mkuu wa polisi Ng’weng’we wa Njagu ili amfungulie Mkumbukwa aliyetiwa mbaroni baada ya kupatikana na begi la unga.
v.Wizi – Vijana mateja wanawaibia watu mitaani
vi.Fujo – Vijana mateja wanazua fujo wakitumia visu na bisibisi
vii.Kudhoofika kwa afya – Afya ya vijana mateja imedhoofika kutokana na matumizi ya unga.Tunaambiwa kwamba hawana nguvu .Wengine wanadondokwa na udenda huku wakiwa wamefumba macho/wengine wamekauka midomo.
viii.Kujitoga mwili – vijana mateja wanajitoga mwili.Mwili umejaa matundu kama jahazi la mtefu.
ix.Kupujuka kwa maadili – Vijana mateja wanawatusi wengine.kwa mfano ,wanamwita mkubwa makande/mavi ya bata
x.Uzembe - Vijana mateja wamekuwa wazembe ;hawafanyi kazi .Wanalaliana vichochoroni baada ya kutumia unga
xi.Vitisho – Unga umewasababisha vijana mateja kuwa wenye vitisho .Kwa mfano,wanamtisha Mkubwa kwamba wangemtoa chango.
xii.Kudhurika kwa akili – Akili za vijana mateja zimevurugika kutokana na matumizi ya unga.Kwa mfano ,kuna kijana mmoja anayemlaumu Mkubwa alipogusa kwamba kwa kufanya hivyo alimwangusha na ndege aliyokuwa akisafiria kuelekeakwa baba Obama ilhali hakuwa akisafiri
xiii.Sober house – Pesa zinazohitajika kuleta maendeleo zinatumika katika kufungua vituo vya kurekebishia tabia za mateja k.v Sober house.
xiv.Magonjwa - Dawa za kulevya zinawasababishia vijana mateja magonjwa kama vile kifua kikuu na ukimwi kutokana na kujitoga mwilini
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:47


Next: Thibitisha kuwa ulitima ni kati ya maudhui ya hadithi ya mkubwa.
Previous: The figure below shows triangle OPQ in which OP = P and OQ = p. M and N are points on OQ and OP respectively...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions