Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi ,’Mapenzi ya kifaurongo’ na ‘Mame Bakari.

      

Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi ,’Mapenzi ya kifaurongo’ na ‘Mame Bakari.

  

Answers


Kavungya
MAPENZI YA KIFAURONGO
i.Wanajamii wanawasaliti wazazi wa Dennis kwa kuwakejeli kwa sababu ya kuwa maskini
ii.Daktari Mbonga anawasaliti wanafunzi kwa kukata kuyajibu maswali yao.Kwa mfano,najibu wanafunzi aliyemuuliza swali kuwa kama hakujua jinsi fasihi inavyoelekeza jamii hakufaa kuwa darasani.
iii.Baadhi ya wanafunzi chuoni Kivukoni wanawasili wenzao kwa kuwacheka wanapomwombaDaktari Mabonga atumie lugha nyepesi msichana mmoja anamcheka mpaka anaanguka
iv.Penina anamsaliti Dennis Machora kwa kumwambia kwamba hawezi kuolewa na mwanamume asiye na kazi yenye mshahara mkubwa ilhali alipomtaka kuwa mchumbawe alimwambia kuwa alichotaka ni uaminifu wa mapenzi tu.
v. Serikali inamsaliti Dennis kwa kutompa ajira.Miaka mitatu ilikuwa imepita akisaka kazi tangu ahitimu masomo yake ya chuo.
vi.Penina anamsaliti Dennis kwa kutombakishia chakula akidai kwamba hakuwa amemwachia
pesa za kununua chakula ilhali alijua kuwa Dennis hakuwa na ajira na alitoka familia maskini.
vii.Penina anamsaliti Dennis kwa kuenda kinyume cha ahadi yake.Anapomtaka Dennis kuwa
mchumba wake anamshawishi moyoni mwake amekuwa na azma ya kumpenda mtu milele lakini anaivunja ahadi hii kwa kuuvunja uchumba wao kwa sababu ya umaskini wa Dennis.
viii.Penina anamsaliti Dennis kwa kumfukuza kutoka kwenye nyumba walikokuwa wakiishi akijua kwamba Dennis hakuwa na uwezo wa kifedha wa kupangisha nyumba kwingine.
ix.Penina anamsaliti Dennis kwa kumdhalilisha .Anapouvunja uchumba wao anamwambia
kwamba asimwite mpenzi na kumshauri amtafute mwingine mwenye hali kama yake (umaskini)
x.Wazazi wake Penina wanamsaliti Dennis kwa kumtahadharisha mwanao Penina dhidi ya kuchumbiwa naye.
xi.Wanafunzi chuoni wanausaliti wajibu wao wa kusoma kwa kuanza kuchumbiana.Kwa mfano,uchumba wa Dennis na Penina.
xii.Dennis na Penina walikuwa wamepanga kuona baada ya kufuzu masomo yao lakini Penina anamsaliti Dennis kwa kuuvunja uchumba wao.
xiii.Penina anawasaliti wazazi wake kwa kutowatii wanapomtahadharisha dhidi ya kuchumbiwa na Dennis – anawapuuza na kuchumbiwa naye.

MAME BAKARI
I. Janadume linamsaliti Sara kwa kumvamia na kumbaka akitoka masomoni
ii.Beluwa anamsaliti Sara kwa kuifichua siri ya mimba yake kwao ilhali alitaka iwe siri
iii.Jamii inamsaliti mwanamke kwa kumwona kuwa mkosaji/shetani tukio la ubakaji linapotokea
iv.Mwalimu mkuu angemsaliti Sara iwapo angemfukuza kutoka shuleni jinsi Sara anavyowazalhali hayakuwa mapenzi yake kubakwa
v.Sara anaona usaliti wa wanajamii kwa sababu anakisia kwamba wangemsusuika na kumtenga kama mgonjwa wa ukoma iwapo wangeujua ujauzito wake ilhali aliupata kutokana na kubakwa.
vi.Baba yake Sara anamsaliti mkewe (mamake SARA)kwa kutompa nafasi ya kujitetea nafsi yake mbele yake.
vii.Sara anauona usaliti wa babake iwapo angejua kuwa yeye ni mjamzito.Sara anaona kuwa baba yake angemfukuza kutoka nyumbani ilhali hakukuwa kupenda kwake kubakwa na kupachikwa mimba.
viii.Raia wanalisaliti janadume lililombaka Sara kwa kuliua kwa matofali licha ya kwamba lilikuwa limemwomba Sara msamaha
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:51


Next: The distance between town A and B is 360km. A minibus left A at 8.15 am and travelled towards B at an average speed of 90km/h....
Previous: “Ndugu yangu kula kunatumaliza” “Kunatumaliza au tunakumaliza” a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Fafanua maana ya kitamthali katika kauli ‘kula tunakumaliza’ c) Kwa mujibu wa hadithi hii, nbi...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions