“Ndugu yangu kula kunatumaliza” “Kunatumaliza au tunakumaliza” a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Fafanua maana ya kitamthali katika kauli ‘kula tunakumaliza’ c) Kwa mujibu wa hadithi hii, nbi...

      

“Ndugu yangu kula kunatumaliza”
“Kunatumaliza au tunakumaliza”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Fafanua maana ya kitamthali katika kauli ‘kula tunakumaliza’
c) Kwa mujibu wa hadithi hii, nbi kwa namna gani wasemaji wanadai kula kunawamaliza?

  

Answers


Kavungya
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
• Kauli ya kwanza ni ya mbura
• Kauli ya apili ni ya sasa.
• Walikuwa nyumbani kwa Mzee Mambo
• Mzee Mambo alikuwa ameandaa hafla ya kusherekea mtoto wake kusajiliwa kwenye shule ya nasari na wa pili meno yalikuwa yamepasua ufizi.
• Wanasema haya baada ya kula sana kwenye sherehe hiyo.

b) Fafanua maana ya kitamthali katika kauli ‘kula tunakumaliza’
• Mzee Mambo kuwa waziri kivuli wa wizara zote – anapokea mshahara lakini hana kazi yoyote.
• Wafanyikazi ni watepetevu-wanafika kazini lakini hafanyi lolote pale kazini.
• Vyeo vya mzee Mmambo vinampa fursa ya kupakuwa mshahara (yeye anachota tu hapewi) uk 37.
• Mzee mambo kuandaa sherehe kubwa ambayo inaangaziwa na vyombo vya habari.
• Wizara moja inaendeshwa na mawazirir wawili – Sasa na Mbura wanadai kuwa wao ni mawaziri wa wizara ya Mipango na mipangilio.
• Sasa na Mbura kuendesha wizara kwa namna ya kujifaidi. Wanasema wizara inawaendesha hasa. Uk 37.
• Magari ya serikali kutumiwa vibaya kwenye sherehe ya Mzee Mambo kuleta jamaa zake, kuleta sherehe havipikwi hapo bali vinaagizwa kwa mali ya umma. Uk 39.
• Mbweo anayoitoa Mbura (uk 40) ni ishara ya shibe aliyonayo. Hizi ni dalili za majitapo/kiburi cha viongozi kuridhika na hali yao ya kuendelea kufaidi kwa wizi wa mali ya uuma.
• Maelezo ya jinsi Sasa na Mbra wanafakamia chakula upsei yanatupa taswira ya jinsi wenye uwezo wanapapia mali ya umma bila kuona haya.
• Mbweo anayoitoa Mbura (uk 40) ni ishara ya shibe aliyonayo. Hizi ni dalili za majitapo/kiburi cha viongozi kuridhika na hali yao ya kuendelea kufaidi kwa wiziz wa mali ya umma.
• Matajiri hawajali lawama kutokana na wizi wao wa mali ya umma.
• DJ kwenue sherehe ya Mzee Mamabo hajali lawama kwa kulipwa mabilioni ya pea kutoka kwenye hazina ya umma.
• DJ ana duka la dawa ambalo mtaji wake ni bohari kubwa ya dawa za serikali.
• DJ na wenzake wanapaata huduma za kimsingi kama vile maji ya umeme huku raia wakiumia.

c) Kwa mujibu wa hadithi hii, nbi kwa namna gani wasemaji wanadai kula kunawamaliza?
• Magonjwa yanayosababishwa na kula lishe isiyobora mfano sukari, presha, saratani, obesti n.k
• Kuna mauaji- watu wanauana kwa kutumia silaha za maangamizi kama vile risasi na mabomu au hata kunyongana kutokana na unyakuzi wa mali ya umma.
• Kuna hai ya kuuna kifikira na kimawazo.
• Uhalifu wa kunyang’anyana mali.
• Kutovukwa na utu/ukosefu wa heshima.
• Kutojirudi kutokana na makosa wafanyayo/kukosa kukiri na kuomba msamaha watendapo maovu.
• Kuhalalisha wizi/unyakuzi – inasemwa kuwa aliyepewa hapokonyeki (ubinafsi)
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:56


Next: Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi ,’Mapenzi ya kifaurongo’ na ‘Mame Bakari.
Previous: “Mame Bakari” Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions