Dhihirisha ukweli wa methali “mzoea sahani vya vigae haviwezi” katika hadithi ya mapenzi ya kifaurongo

      

Dhihirisha ukweli wa methali “mzoea sahani vya vigae haviwezi” katika hadithi ya mapenzi ya kifaurongo

  

Answers


Kavungya
i. Mtu ambaye ni tajiri mwenye kuzoea kuwa na mahitaji yote maishani kama penina itakuwa vigumu kuishi kwa taabu na hali ambayo kila kitu ni duni.
ii. Penina Anatoka katika familia yenye nafsi kifedha, hivyo hakosi mahitaji yake yote. Masurufu yake yalikuwa shilingi elfu tano kila juma.
iii. Dennis ni mtoto wa fukara ambaye amekosa mahitaji yake ya msingi. Hata chakula anapata kwa shida sana.
iv. Dennis anaona haitawezekana kuwepo na mahusiano mwafaka kati ya Penina.
v. Penina anasisitiza kuwa inawezekana kabisa msichana wa kitajiri atangamane na kijana mwanaume ambaye ni fukara.
vi. Penina anafanikiwa kumshawishi Dennis kwamba hilo linawezekana na wanaanza kuwa na uhusiano wa kimapenzi.
vii. Waliahidiana kuwa wangefunga ndoa baada ya kuhitimu masomo yao na kupata kazi.
viii. Walishirikiana vema na wakaonyesha mapenzi moto moto mithili yao ulimi na mate.
ix. Walipomaliza masomo waliamua kuishi pamoja katika nyumba ya kupanga. Kila kitu waligharimiwa na wazazi wake Penina.
x. Baadaye changamoto inaibuka wakati Penina anapodai kuwa hawezi kuolewa na mwanaume ambaye hana kazi yenye mshahara mkubwa.
xi. Penina anamvumilia Dennis kwa muda wa miaka mitatu na hatimaye uvumilivu unamshinda.
xii. Ahadi zote ambazo Penina alimuahidi Dennis zikaanza kuota mbawa.
xiii. Penina anamfukuza Dennis kwenye nyumba wanamoishi kwa kuwa amekosa kazi na hana msaada wowote kwake zaidi ya kumnyonya tu.
xiv. Penina anaweka bayana kabisa kuwa pasipo matunzo mwafaka mapenzi yake kwa Dennis yanashindwa kustawi.
Mgomba changaraweni haustawi.
xv. Kwa hiyo ni ukweli kabisa kuwa mzoea vya sahani, vya vigae haviwezi kwa sababu Penina aliyekuwa amezoea maisha ya raha anashindwa kukubaliana na dhiki anayokumbana nayo baada ya kuishi na Dennis.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 08:05


Next: Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa Madongo poromoka katika tumbo lisiloshiba
Previous: The diagram below shows a frustum which represents a bucket with an open top diameter of 30cm and a bottom diameter of 24cm. The bucket is...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions