Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Hakuchukua muda mrefu, akili zao zilipowaamsha kuwapeleka kwenye maana hasa ya kile kilichokuwa kikitokea ...” a. Eleza muktadha wa dondoo hili b. Fafanua tamathali ya usemi aliyoitumia...

      

“Hakuchukua muda mrefu, akili zao zilipowaamsha kuwapeleka kwenye maana hasa ya kile kilichokuwa kikitokea ...”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
b. Fafanua tamathali ya usemi aliyoitumia mwandishi katika dondoo hili
c. Fafanua kile kilichokuwa kikitokea
d. Eleza juhudi zilizofanywa kuzuia kilichokuwa kikitokea kisitoke

  

Answers


Kavungya
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
Mnenaji – msimulizi
Mnenewa – anawarejelea wenyeji wa Madongoporomoka
Mahali – vibandani katika eneo la Madongoporomoka
Sababu – Mabuldoza yalikuwa yameanza kubomoa vibanda vya watu wa Madongoporomoka

b. Fafanua tamathali ya usemi aliyoitumia mwandishi katika dondoo hili
Tashihisi Akili zao zilipowaamsha kuwapaleka kwenye maana hasa

c. Fafanua kile kilichokuwa kikitokea
Vibanda vya watu wa Madongoporomoka
Jeshi la polisi lililokuwa limeshika bunduki lilisimamia mabuldoza yakibomoa vibanda
Watu waliokuwa wamelala walitimuliwa
Askari wa baraza la jiji walikuwa wanabomoa vibanda
Kulikuwa na muangaiko hasa kwa watu wa Madongoporomoka

d. Eleza juhudi zilizofanywa kuzuia kilichokuwa kikitokea kisitoke
o Watu walikuwa wanafanya kikao katika hoteli yam mzee Mago kujadili namna ya kuzuia kubomolewa vibanda vyao
o Kutafuta wanasheria waaminifu ili kutatua sitofahamu
o Mzee Mago alishinda kuwazindua Wanadongoporomoka kuchunguza maendeleo yanayozungumziwa kama yangeleta manufaa au hasara
o Mzee Mago aliwaleta watu Madongoporomoka pamoja ili kutetea haki ya kumiliki ardhi yaMadongoporomoka
o Kabwe alisisitiza kwa nguvu kuwa wakubwa hawangeweza, kwani wanaongopa umma wa Madongoporomoka
o Wanyonge walishikilia kauli yao kuwa fujo zisingeweza kuwaondoa katika ardhi yao
o Baada ya majuma matatu ya vurugu vibanda mshenzi vya Madongoporomoka viliota tena vingi kuliko vya awali
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 08:11


Next: Aliyeumwa na nyokaakiona ung’ong’o hushtuka a) Weka dondoo hili katika muktadha b) Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka c) Mzungumziwa anaendeleza vipi maudhui ya ushauri na ukosefu wa...
Previous: Ulezi umewapa wazazi wengi changamoto nyingi. Ukirejelea hadithi ya shogake, dada ana ndevu dhihirisha ukweli wa kauli hii

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions