a) Eleza muktadha wa dondoo hili
Haya ni maneno ya Lulua.
Anamwambia mamake Bi.Hamida.
Wamo nyumbani mwao wakila chamcha.
Lulua anamweleza jinsi alivyoingia katika chumba cha Safia na kumkuta akiwa amelala kitandani na Kimwana.
b) Bainisha sifa tatu za ‘shoga’ anayezungumziwa katika dondoo hili.
(i)Misri-Wazazi wake Safia hawakuwahi kuiona sura yake kwa sababu alipenda kuvaa buibui ili asijulikane kuwa ni mwanamume.
(ii)Mzinifu-Anazini na Safia na kumpachika mimba.
(iii)Mjanja-Anajifunika buibui na kujifanya jinsia ya kike.
c) Jadili umuhimu wa ‘dada’ anayerejelewa katika kuendeleza dhamira ya hadithi.
Dada anayerejelewa ni Safia.Ana umuhimu ufuatao:
(i)Ametumiwa kudhihirisha maana ya methali:`mtu huvuna apandacho.’Anazini na Kimwana anayempachika mimba .Anajaribu kuiavya mimba hiyo lakini ankufa.
(ii)Ni kiwakilishi cha uozo katika jamii.Anawahadaa wazazi wake kuwa Kimwana ni shogake kumbe ni mpenziwe wa kiume.
(iii)Ametumiwa kukosoa malezi ya wazazi.Wazazi wake Bwana Masudi na Bi Hamida walimwamini sana hadi wakawa wanamsifu tu badala ya kuzungumza naye ili kumpa mwelekeo ufaao maishani.
(iv)Ametumiwa kubainisha maana ya methali:`Si vyote ving’aavyo ni dhahabu.’Alionekana kwa wazazi wake kuwa motto mwadilifu mpaka waka wanamsifu tu na kumshukuru Mola kwa kuwajalia motto kama huyo kumbe alikuwa mwovu.
(v)Kuendeleza maudhui ya elimu.Alikuwa mwerevu shuleni.Kila mtihani alioufanya aliongoza katika darasa lao.
(vi)Ametumiwa kudhihirisha maana ya methali:`Nyumba nzuri si mlango fungua uingie ndani.’Wazazi wake wamekuwa wakimsifu Safia tu bila kumchunguza ili kujua mienendo yake.Wanakuja kugundua uovu wake baadaye wakati alikuwa ashaavya mimba na kuaga dunia.
(vii)Ni kielelezo cha wanawake wanaoavya mimba ili kuuficha uovu huo.Safia anajaribu kuavya mimba ili wazazi wake wasijue lakini anakufa.
(viii)Suala la unafiki linajitokeza kupitia kwake.Alijifanya mzuri kwa wazazi wake hadi wakamwamini kwa kila jambo kumbe alikuwa mwovu-anawahadaa wazaziwe kuwa Kimwana ni shogaye ilhali ni mpenziwe wa kiume.
(ix)Ni kielelezo cha athari za mapenzi kabla ya ndoa.Anafanya mapenzi na Kimwana.Anapachikwa mimba na kwa sababu ya kuhofia matokeo yake anaamua kuiavya ili iwe siri lakini anakufa.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 08:17
- Fafanua jinsi mwandishi wa ‘Tumbo Lisiloshiba’ alivyotumia kinaya kufanikisha maudhui yake(Solved)
Fafanua jinsi mwandishi wa ‘Tumbo Lisiloshiba’ alivyotumia kinaya kufanikisha maudhui yake
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Fafanua changamoto zinazokabili asasi ya ndoa ukirejelea hadithi ya Masharti ya kisasa(Solved)
Fafanua changamoto zinazokabili asasi ya ndoa ukirejelea hadithi ya Masharti ya kisasa
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Ulezi umewapa wazazi wengi changamoto nyingi. Ukirejelea hadithi ya shogake, dada ana ndevu dhihirisha ukweli wa kauli hii(Solved)
Ulezi umewapa wazazi wengi changamoto nyingi. Ukirejelea hadithi ya shogake, dada ana ndevu dhihirisha ukweli wa kauli hii
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “Hakuchukua muda mrefu, akili zao zilipowaamsha kuwapeleka kwenye maana hasa ya kile kilichokuwa kikitokea ...”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
b. Fafanua tamathali ya usemi aliyoitumia...(Solved)
“Hakuchukua muda mrefu, akili zao zilipowaamsha kuwapeleka kwenye maana hasa ya kile kilichokuwa kikitokea ...”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
b. Fafanua tamathali ya usemi aliyoitumia mwandishi katika dondoo hili
c. Fafanua kile kilichokuwa kikitokea
d. Eleza juhudi zilizofanywa kuzuia kilichokuwa kikitokea kisitoke
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Aliyeumwa na nyokaakiona ung’ong’o hushtuka
a) Weka dondoo hili katika muktadha
b) Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka
c) Mzungumziwa anaendeleza vipi maudhui ya ushauri na ukosefu wa...(Solved)
Aliyeumwa na nyokaakiona ung’ong’o hushtuka
a) Weka dondoo hili katika muktadha
b) Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka
c) Mzungumziwa anaendeleza vipi maudhui ya ushauri na ukosefu wa utu?
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Dhihirisha ukweli wa methali “mzoea sahani vya vigae haviwezi” katika hadithi ya mapenzi ya kifaurongo(Solved)
Dhihirisha ukweli wa methali “mzoea sahani vya vigae haviwezi” katika hadithi ya mapenzi ya kifaurongo
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa Madongo poromoka katika tumbo lisiloshiba(Solved)
Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa Madongo poromoka katika tumbo lisiloshiba
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “Masharti ya Kisasa”
“…mapenzi ni mateso,ni utumwa, ni ukandamizaji , ni ushabiki usio na maana.”
Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi.(Solved)
“Masharti ya Kisasa”
“…mapenzi ni mateso,ni utumwa, ni ukandamizaji , ni ushabiki usio na maana.”
Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “Mame Bakari”
Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka.(Solved)
“Mame Bakari”
Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “Ndugu yangu kula kunatumaliza”
“Kunatumaliza au tunakumaliza”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Fafanua maana ya kitamthali katika kauli ‘kula tunakumaliza’
c) Kwa mujibu wa hadithi hii, nbi...(Solved)
“Ndugu yangu kula kunatumaliza”
“Kunatumaliza au tunakumaliza”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Fafanua maana ya kitamthali katika kauli ‘kula tunakumaliza’
c) Kwa mujibu wa hadithi hii, nbi kwa namna gani wasemaji wanadai kula kunawamaliza?
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi ,’Mapenzi ya kifaurongo’ na ‘Mame Bakari.(Solved)
Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi ,’Mapenzi ya kifaurongo’ na ‘Mame Bakari.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- “ Naapa na mola wangu sitofanya tena biashara hii.”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
b. Tathmini umuhimu wa mzungumzaji
c. “Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa...(Solved)
“ Naapa na mola wangu sitofanya tena biashara hii.”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
b. Tathmini umuhimu wa mzungumzaji
c. “Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa jamii.” Huku ukirejelea hadithi hii,thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Thibitisha kuwa ulitima ni kati ya maudhui ya hadithi ya mkubwa.(Solved)
Thibitisha kuwa ulitima ni kati ya maudhui ya hadithi ya mkubwa.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Mhini na mhiniwa njia yao moja. Jadili ukweli wa methali hii ukirejelea hadithi ya mkubwa(Solved)
Mhini na mhiniwa njia yao moja. Jadili ukweli wa methali hii ukirejelea hadithi ya mkubwa
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili
c)...(Solved)
Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili
c) Fafanua sifa za msemaji
d) Jadili maudhui ya utabaka ukjirejelea hadithi husika.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika ‘Tumbo lisiloshiba na Hadithi nyingine’, fafanua maudhui ya utabaka.(Solved)
Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika ‘Tumbo lisiloshiba na Hadithi nyingine’, fafanua maudhui ya utabaka.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Huku ukirejelea hadithi za:
i) Mapenzi ya kifaurongo
ii) Shogake dada ana ndevu
iii) Mame Bakari
Fafanua maudhui ya mapenzi kama yanavyosawiriwa.(Solved)
Huku ukirejelea hadithi za:
i) Mapenzi ya kifaurongo
ii) Shogake dada ana ndevu
iii) Mame Bakari
Fafanua maudhui ya mapenzi kama yanavyosawiriwa.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Fafanua sifa kumi za mzee Mago katika hadithi ya tumbo lisiloshiba.(Solved)
Fafanua sifa kumi za mzee Mago katika hadithi ya tumbo lisiloshiba.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Anwani ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni mwafaka kwa hadithi hii. Fafanua(Solved)
Anwani ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni mwafaka kwa hadithi hii. Fafanua
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)
- Kwa kurejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na ya Mapenzi ya Kifaurongo, fafanua maudhui ya utabaka.(Solved)
Kwa kurejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na ya Mapenzi ya Kifaurongo, fafanua maudhui ya utabaka.
Date posted: May 6, 2019. Answers (1)