Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

‘… lakini shogake… shogake… shogake dada nikamwona ana ndevu.’ a) Eleza muktadha wa dondoo hili b) Bainisha sifa tatu za ‘shoga’ anayezungumziwa katika dondoo hili. c) Jadili umuhimu...

      

‘… lakini shogake… shogake… shogake dada nikamwona ana ndevu.’
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Bainisha sifa tatu za ‘shoga’ anayezungumziwa katika dondoo hili.
c) Jadili umuhimu wa ‘dada’ anayerejelewa katika kuendeleza dhamira ya hadithi.

  

Answers


Kavungya
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
Haya ni maneno ya Lulua.
Anamwambia mamake Bi.Hamida.
Wamo nyumbani mwao wakila chamcha.
Lulua anamweleza jinsi alivyoingia katika chumba cha Safia na kumkuta akiwa amelala kitandani na Kimwana.

b) Bainisha sifa tatu za ‘shoga’ anayezungumziwa katika dondoo hili.
(i)Misri-Wazazi wake Safia hawakuwahi kuiona sura yake kwa sababu alipenda kuvaa buibui ili asijulikane kuwa ni mwanamume.
(ii)Mzinifu-Anazini na Safia na kumpachika mimba.
(iii)Mjanja-Anajifunika buibui na kujifanya jinsia ya kike.

c) Jadili umuhimu wa ‘dada’ anayerejelewa katika kuendeleza dhamira ya hadithi.
Dada anayerejelewa ni Safia.Ana umuhimu ufuatao:
(i)Ametumiwa kudhihirisha maana ya methali:`mtu huvuna apandacho.’Anazini na Kimwana anayempachika mimba .Anajaribu kuiavya mimba hiyo lakini ankufa.
(ii)Ni kiwakilishi cha uozo katika jamii.Anawahadaa wazazi wake kuwa Kimwana ni shogake kumbe ni mpenziwe wa kiume.
(iii)Ametumiwa kukosoa malezi ya wazazi.Wazazi wake Bwana Masudi na Bi Hamida walimwamini sana hadi wakawa wanamsifu tu badala ya kuzungumza naye ili kumpa mwelekeo ufaao maishani.
(iv)Ametumiwa kubainisha maana ya methali:`Si vyote ving’aavyo ni dhahabu.’Alionekana kwa wazazi wake kuwa motto mwadilifu mpaka waka wanamsifu tu na kumshukuru Mola kwa kuwajalia motto kama huyo kumbe alikuwa mwovu.
(v)Kuendeleza maudhui ya elimu.Alikuwa mwerevu shuleni.Kila mtihani alioufanya aliongoza katika darasa lao.
(vi)Ametumiwa kudhihirisha maana ya methali:`Nyumba nzuri si mlango fungua uingie ndani.’Wazazi wake wamekuwa wakimsifu Safia tu bila kumchunguza ili kujua mienendo yake.Wanakuja kugundua uovu wake baadaye wakati alikuwa ashaavya mimba na kuaga dunia.
(vii)Ni kielelezo cha wanawake wanaoavya mimba ili kuuficha uovu huo.Safia anajaribu kuavya mimba ili wazazi wake wasijue lakini anakufa.
(viii)Suala la unafiki linajitokeza kupitia kwake.Alijifanya mzuri kwa wazazi wake hadi wakamwamini kwa kila jambo kumbe alikuwa mwovu-anawahadaa wazaziwe kuwa Kimwana ni shogaye ilhali ni mpenziwe wa kiume.
(ix)Ni kielelezo cha athari za mapenzi kabla ya ndoa.Anafanya mapenzi na Kimwana.Anapachikwa mimba na kwa sababu ya kuhofia matokeo yake anaamua kuiavya ili iwe siri lakini anakufa.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 08:17


Next: A piece of wire can be folded into a rectangle whose dimensions are such that its length is 3cm longer than the width. The area of...
Previous: A survey recorded the measurement of a field book using XY = 400m as the base line as shown below.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions