``Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini…’’ a)Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. c) Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili kinachorejelewa...

      

``Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini…’’
a)Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili.
c) Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili kinachorejelewa katika dondoo hili.
d) Eleza wasifu wa warejelewa katika dondoo hili.

  

Answers


Kavungya
a)Eleza muktadha wa dondoo hili.
Hii ni kauli ya mwandishi
ii) anarejelea tukio la ulafi wa Jitu
iii) mahali ni katika mkahawa mshenzi wa Mzee Mago
iv) watu wamepigwa na butwaa kwa tendo la ulafi wa Jitu

b) Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili.
i) nahau- kukiangua kitendawili
ii) jazanda - neno `kitendawili’ kurejelea jambo fulani lililofichika

c) Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili kinachorejelewa katika dondoo hili.
)Kuwepo kwa uvumi na nong`ono kuhusu uwezekano wa kunyakuliwa ardhi ya Wanamadongoporomoka.
ii)Mzee Mago kuwahamasisha raia kuhusu haja ya kutetea kazi zao.
iii)Mikutano ya kuandaa mikakati ya kutetea haki za Wanamadongoporomoko inayofanyika katika mkahawa.
iv)Jitu kuwasili mkahawa mshenzi na kuzua taharuki
v)Jitu kuamrisha kuhudumiwa na kula chakula chote kilichoandaliwa.
vi)Watu kupigwa na butwaa kwa ulafi wa jitu na kuwazia tendo hili
Hatima
- Jitu kuahidi kurudi keshoye kula maradufu ya siku hiyo.
i)Hatimaye jitu kufika na mabuldoza
ii)Askari wa baraza kuandamana na jitu
iii)Jeshi la polisi kuwalinda askari wa baraza
iv)Watu kupigwa virungu bila hatia
v)Vibanda kubomolewa
vi)Watu kujenga upya` vibanda mshezi’ zaidi ya hapo awali

d) Eleza wasifu wa warejelewa katika dondoo hili.
i)Wazalendo halisi; wanaendeleza harakati za kupigania haki zao za kumiliki na kukomboa ardhi yao.
ii)Wenye bidii: hawasiti /hawakomi kuandaa mikakati ya kupigania haki zao . mfano: mikutano yao.
iii)Wenye umoja na ushirikiano : wanashirikiana kwa kukutana na kupanga utetezi wa haki zao.
iv) Wakakamavu/ jasiri: wanakaidi hatua ya Jitu na kuikomboa ardhi yao iliyonyakuliwa.
v)Wenye hekima/ busara: wanabaini hila za wenye nguvu kutaka kunyakua ardhi yao na kujiandaa kukabiliana nao.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 08:20


Next: A survey recorded the measurement of a field book using XY = 400m as the base line as shown below.
Previous: Use logarithm tables to evaluate

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions