Kidagaa Kimemwozea: "Wasemao husema, atafutaye hachoki." (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Kauli hii ina tnaana gani kwa mujibu wa muktadha huu. (c) Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika...

      

Kidagaa Kimemwozea:
"Wasemao husema, atafutaye hachoki."
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Kauli hii ina tnaana gani kwa mujibu wa muktadha huu.
(c) Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa
Kimemwozea.

  

Answers


Kavungya
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
Majuhuni aliyejitahidi kumfurahisha mpenziwe Mitchelle aliyekuwa
amekataa kuolewa naye mpaka ajenge jumba la kifahari. Licha ya jitihada
zake Majununi, Mitchelle alikataa kuolewa na Majununi na baadaye
Maajununi akaamua kutooa kamwe.

(b) Kauli hii ina tnaana gani kwa mujibu wa muktadha huu.
Majununi hakufa moyo katika harakati za kutaka kumwoa Mitchelle.
Alijitahidi kutimiza matakwa ya mpeni wake kwa kujenga nyumba nyingine.

(c) Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa
Kimemwozea.
- Imani anatafuta haki ya kunyimwa malezi ya wazazi wake waliouliwa
kinyama. Imani anatafuta haki ya familia yake iliyonyanganywa shamba
lao.
- Amani anatafuta haki ya Ami yake Yusufu.
- DJ anatafuta haki baada ya kushambuliwa na jibwa lake Nasaba Bora.
- Amani anatafuta haki ya mswada uiiokataliwa na wachapishaji na baadaye
kuchapishwa kwa jina la mtu mwingine.
- Chwechwe Makweche anatafuta haki ya kuumia michezoni bila kufidiwa.
- Watoto wa Majisifu wanalilia haki ya kuishi kama binadamu wengine licha
ya ulemavu wao. Amani anatafuta haki ya kudhulumiwa na mtemi Nasaba
Bora kwa kizingizio kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mkewe Bi
Zuhura. Amani atafuta haki ya kujua waliokuwa wazazi wa kitoto Uhuru
baada ya yeye kulazimishwa kukilea licha ya kuwa hakuwa babake. Amani
na Imani wanatafuta haki ya kufungwa kwa kizingizio kuwa walimwuua
mtoto Uhuru. Wanafunzi wa mwalimu Majisifu wanatafuta haki ya kufunzwa
vyema baada ya Mwalimu wao kutohudhuria shule kwa muda mrefu. Yusufu
anatafuta haki baada ya kusingiziwa kumwuua Chichiri Hamadi.
- Raia wa Sokomoko wanatafuta haki dhidi ya Nasaba Bora anayewapokonya
ardhi, mali, mabiruti na wake wao.
- Wafungwa wanatafuta haki kwa kukosa kufikishwa mahakamani.
- Waandishi wengi chipukizi kama Amani wanatafuta haki ya kazi zao baada
ya kuibiwa miswada yao na akina Majisifu.
Kavungya answered the question on May 7, 2019 at 08:34


Next: List the Personal, Health, Effects and Economic effects of drug abuse.
Previous: What is the solution of drug Abuse?

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions