Damu Nyeusi Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa "Kanda la Usufi", "Shaka ya Mambo" na "Tazama na Mauti"

      

Damu Nyeusi
Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa "Kanda la Usufi", "Shaka ya Mambo"
na "Tazama na Mauti"

  

Answers


Kavungya
- Shule imesawiriwa kama mahali pa kuadilisha wanafunzi.
- Kuhakikisha kuwa wanafunzi wamo katika hali nzuri ya kiafya ili kuendeiea
katika masomo -mfano - desturi ya shule ya Askofu Timotheo kuwachunguza
wasichana wote kama wana mimba.
- Matokeo ya vitendo vya wanafunzi yanadhihirika katika hadithi tofauti.
Katika Kanda la Usufi, Sela na Masazu hawafanyi vyema kwenye mtihani
- Katika Tazamana na Mauti, ukosefu wa hamu ya masomo unamfanya Lucy
asifanye vyema kwenye mtihani.
- Wazazi hukatatam-aa watoto wao wanapoenda kinyume na matarajio yao.
- Elimu pia humpa binadamu uhuru kujipangia mustakabadhi wake.
- Masazu anapata kazi ya kijungu jiko huku Sela akitamani kumchukua mtoto
wake ajilele kwa vile hakuwa na la kufanya Masazu anapoenda kazini
- Katika Kanda la Usufi imeelezwa kuwa wasichana walitarajiwa kuendeleza
shughuli zao kwa utulivu na ustaarabu huku wakizingatia maadili ya hali ya
juu. Elimu pia inatarajiwa kuwapa wanafunzi nafasi ya kukuza vipaji vyao
na kuingiliana ili kuelewana zaidi.
- Jukumu la mwanafunzi katika masomo limejitokeleza Bi Margaret mwalimu
mkuu wa shule ya Askofu Timotheo anapowahutubia wanafunzi na kusisitiza
uwajibikaji katika vitendo vyao.
- Katika Tazamana na Mauti Lucy anaamini kuwa jiji hili lina raha kamili bila
karaha.
- Anategemea mzungu atakayemwoa na kumpeleka London na baadaya
kufika London akaanza kutegemea kifo cha Bw. Crusoe ambacho kingempa
urithi na raha aliyotaka maishani
- Hili linadhihirika wakati mzee Butali anapomwuliza mwalimu kwa nini
wazazi huwapeleka watoto shuleni.
- Ukosefu wa elimu umeonyeshwa kama mojawapo ya njia zinazowapa vijana
mitazamo finyu kuhusu maisha.
- Esther katika Shaka ya Mambo alijua alichokuwa akitafuta.
- Kwa upande mwingine mustakabali wa Lucy ulitegemea wengine.
- Alikuwa amepanga ni kwa muda gani angeendelea kufanya kazi jinsi
atakavyopanga wakati wake baada ya kujiunga na chuo kikuu na
anachotaka kusomea.
Kavungya answered the question on May 7, 2019 at 08:49


Next: Given that log of 7 = 0.8451 and log of 6 = 0.7782. Find log of 25.2
Previous: What are the recommendations of family planning?

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions