MUHTASARI (alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima...

      

MUHTASARI (alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa
kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima sawa. Utaifa hujengwa kwenye
misingi ya mapenzi kwa nchi, Utambuzi wa cheo, eneo, hadhi, rangi na hata
makabila wanakotoka raia wa taifa moja si chanzo cha kuwatanganisha. Nchi moja
huweza kuundwa na watu walio na tofauti chungu nzima zikiwemo tofauti za
kikabila, kitabaka na kimawazo. Hata hivyo, watu hao huwa na folsafa na imani
sawa kama taifa inayoashiriwa hasa na wimbo wa taifa. Hata hivyo haya yotc
hayawezi kuwafikia katika kiwango cha kuunda taifa. Uzalendo ndio mhimili
mkuu wa utaifa. Uzalendo ni mapenzi aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Mapenzi
haya humwongoza mtu katika mawazo yake, itikadi yake, matendo yake,
matamanio yake na mkabala wake kuhusu nchi na hatima ya nchi yake.
Mzalendo hawezi kushiriki katika matendo yanayoweza kuiletea nchi yake
maangamizo kwa vyovyote vile. Mzalendo huongozwa na mwenge wa wema.
Mzalendo hawezi kushiriki kwenye shughuli zozote zinazohujumu mshikamano wa
kitaifa. Yeye hatawaliwi na ubinafsi wa kutaka kufaidi nafsi yake naya jamii
yake finyu. Matendo yake yote huongozwa na ari ya kuiboresha nchi yake.
Anayeipenda nchi yake hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mali. Yuko radhi
kuhasirika mradi taifa lake linufaike.
Utaifa ni mche aali unaopaliliwa kwa uzalendo, kuepuka uchu wa nafsi na taasubi
hasi zikuwepo za kikabila na ubinafsi. Hali hii inapofikiwa, hatima ya taifa na
mustakabali wa raia wake huwa wenye matumaini makubwa.
(a) Kwa maneno 40 - 50 dondoa sifa kuu za utaifa.
(b) Ni nini misingi ya kutathmini mzalendo? (maneno 60 - 70)

  

Answers


Kavungya
(a) Kwa maneno 40 - 50 dondoa sifa kuu za utaifa.
- Kuwepo kwa hatima sawa
- Kuwepo kwa maono sawa
- Kuwepo kwa falsafa/imani/itikadi sawa.
- Kuwepo kwa mwelekeo mmoja.
- Umejengwa kwa hisia za mapenzi kwa nchi.

(b) Ni nini misingi ya kutathmini mzalendo? (maneno 60 - 70)
- Hawezi kushiriki kwenye shughuii zozote zinazohujumu mshikamano wa
kitaifa.
- Hawezi kutawaliwa na ubinafsi
- Hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mali.
- hawezi kutenda mambo ya kuiletea nchi yakemaangamizo.
- Yuko radhi kuhasirika kwa manufaa ya taifa lake.
- Matendo yake huongozwa na mwenge wa wema.
- Matendo yake huongozwa na ari kuiboresha nchi yake.
Kavungya answered the question on May 7, 2019 at 11:53


Next: PQRS is a cyclic quadrilateral and O is the centre of the circle. angle QOS = 1500
Previous: The angle subtended by the major arc at the centre of the circle O is twice the angle subtended by the minor arc at the centre....

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions