UFAHAMU Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi yanayoendelea...

      

UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni
kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi
yanayoendelea na kuyatosa kwenye shida nyingi huku mataifa ya magharibi
yakizidi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo. Tofauti iliyopo kati ya mataifa
yanayoendelea na yaliyoendelea inaendeiea kuongezeka kila siku.
Miongoni mwa sababu zinazochangia katika ufukara huu ni pamoja na ufisadi,
uongozi mbaya, turathi za kikoloni na uchumi unaotegemea kilimo ambacho
hutegemea mvua isiyoweza kutabirika. Vilevile, mataifa yanayoendelea yana idadi
kubwa ya watu inayoupiku uwezo wa mataifa husika. Pamoja na haya, mataifa
haya hayana uwezo wa kuwakomboa raia wake kutoka katika lindi la umaskini
huu unaokithiri. Ukosefu wa elimu na nafasi adimu za kazi huchangia pia katika
tatizo hili. Ni wazi kuwa ufukara una athari hasi kote ulimwenguni. Aghalabu,
ufukara huchipuza matendo mabaya. Ni rahisi kuwashawishi wananchi maskini
kushiriki katika uhalifu iii kujinasua kutoka kwenye lindi la kimaskini. Udhaifu huu
huweza kuzaa mbegu ya kuatika maovu ya kila aina ukiwemo ugaidi. Mataifa
yaliyoendelea yanatakiwa kuyaburai madeni yanayoyadai mataifa yanayoendelea
kama njia moja ya kupambana na ufukara. Mataifa haya maskini hutumia asilimia
kubwa ya mapato ya kitaifa kuyalipia madeni haya. Hali hii imeyafanya mataifa
haya kushindwa kujikwamua kutoka kwenye minyororo ya ufukara. Njia nyingine
ya kuyasaidia mataifa haya ni kukubali kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya
mikopo kwa nchi husika.
Mataifa yanayoendelea nayo yanatakiwa kuchukua hatua katika kuwanusuru raia
wake kutoka kwenye dhiki hii.Ni sharti yaibuke na mikakati kabambe ya
kupambana na ufukara. Itakuwa na faida kubwa iwapo mataifa haya yataunda
sera zinazotambua ufukara kama tatizo kuu linalozikabili na kuweka mikakati ya
kuwaokoa raia wake kutoka kwenye tatizo hili. Pamoja na mikakati hii ni kuzalisha
nafasi za kazi, kuimarisha miundo msingi,kuendeleza elimu inayolenga kutatua
matatizo maalumu katika jamii na kupanua viwanda. Kuna pia haja ya viongozi
kuwa waangalifu ili mfumo wa soko huru ambao unaendelezwa na mataifa
yaliyoendelea usiishie kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia. Maamuzi yote ya
sera za kiuchumi sharti yauzlngatie uhalisia wa maisha ya raia wa mataifa haya.
(a) Eleza athari za madeni kwa nchi zinazoendelea.
(b) Kwa nini umaskini unatawala mataifa yanayoendelea?
(c) Mwandishi anatoa mapendekezo yapi kwa mataifa yanayoendelea katika
kutatua tatizo la ufukara?
(d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa yanayoendelea?
(e) Taja visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu.
(i)Turathi za kikoloni
(ii) Kuatika
(iii) Kuyaburai

  

Answers


Kavungya
(a) Eleza athari za madeni kwa nchi zinazoendelea.
- Asilimia kubwa ya patu la mataifa yanayoendelea huishia kulipa madeni
haya.
- Hivyo inakuwa vigumu kwa mataifa hayo hujikwamua kutokana na
umaskini.
(b) Kwa nini umaskini unatawala mataifa yanayoendelea?
- Ufisadi, uongozi mbaya, turathi za kikoloni, uchumi kutegemea kilimo chenye
mvua isiyotabirika, idadi kubwa ya watu, nafasi adimu za kazi, madeni na
ukosefu wa elimu
(c) Mwandishi anatoa mapendekezo yapi kwa mataifa yanayoendelea katika
kutatua tatizo la ufukara?
- Kuibuka na mikakati bora ya kupambana na umaskini.
- Sera zinazotambua kuwa raia wake wengi ni maskini.
- Kuzalisha nafasi za ajira kuimarisha miundo msingi.
- Kuendeleza elimu inayolenga kutatua matatizo maalum
- Kupanua viwanda.
- Kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huu hauishii kusababisha kufungwa kwa
viwanda.
(d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa yanayoendelea?
Unaweza kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia.
(e) Taja visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu.
(i)Turathi za kikoloni
Masalio ya kikoioni/ukoloni mambo Ieo / athari za ukoloni.
(ii) Kuatika
Kuzalisha/kuwa
chanzo/kuanzisha/kuleta/kusababisha/kupanda.
(iii) Kuyaburai
Kuyasarnehe/kuyaondoa/kuyasahau/kuyapuuza/kuyafutilia mbali
Kavungya answered the question on May 7, 2019 at 12:02


Next: Determine the values of m for which the matrix below has no inverse
Previous: Rewrite each of the sentences below to make it communicate more sensibly. (i) Powerful and comfortable the buyer really liked the car. (The buyer really liked the...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions